KUMRADHI...
MABADILIKO KIDOGO YA RATIBA YA MUDA WA MAZISHI
Kwa niaba ya Familia ya Mama Salma Rashid-Kikwete na Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, nasikitika kutoa taarifa kuwa jana Alhamisi Julai 19, 2018 Mama Salma Rashid Kikwete amefiwa na Baba yake Mzazi, Mzee Rashid Mkwachu, katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.Shughuli za Msiba zitakuwa nyumbani kwa Mama na Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Msasani jijini Dar es salaam.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika katika makaburi ya Kisutu leo Ijumaa Julai 20, 2018 Saa tisa kabla ya Swala ya Alasiri (kunradhi, sio saa 10 kama ilivyotangazwa awali). Kisomo na dua vitafanyika hapo Msasani kabla ya Swala ya Ijumaa.
Kwa niaba ya Familia
Ridhiwani Kikwete
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...