JOSEPH MPANGALA -MTWARA.
Serikali
imesema Imefuta Mpango wa Kufanya Elimu ya Msingi Kuishia darasa la
Sita Kutokana na Kuonekana Mfumo wa Kuishia Darasa la Saba Hauna
matatizo Yoyote na Umeendelea Kufanya Vizuri kwa Wanaomaliza.
Hayo
yamesemwa na Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Ole
Nasha mara baada ya Kumaliza kutembelea Chuo cha Ualimu Kitangali
Kilichopo Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara.Ole
Nasha Amesema Mpango wa Elim ya Msingi Kuishia darasa la Sita Ulikuwepo
lakini baada ya Kupokea mawazo Wameamua Kuacha kama Ilivyo.
“Kulikuwa
na Mpango wa kujaribu kufanya sasa Elimu ya msingi iishie darasa la
Sita iwe miaka sita lakini kwa sasa hakuna huo Mpango tumerudi kwenye
mfumo wetu wa kawaida kwa sababu moja tu hakuna kitu kilicho haribika,
kila mtu aliyesoma Nchi hii amesoma kwa mfumo ule hatujaona kama
unamapungufu yoyote kwa hiyo tutaendelea na utaratibu wetu wa Miaka
Saba”amesema Ole Nasha
Aidha
Naibu waziri amewataka Makandarasi wanaojenga Katika Mradi wa Chuo Cha
Kitangali Kuhakikisha wanamalizia Ujenzi Pindi watakapo pata Pesa Kutoka
serikalini.
“Mimi
ninaloondoka nalo hapa ni kwenda kuhakikisha kwamba Fedha Yaani
Certificate hizo ambazo zimetoka karibuni kwamba zinalipwa mapema, Rai
yangu kwenu Jamani Mradi huu umechukua muda mrefu,karibia miaka miwili
kwa hiyo fedha zikilipwa kila mmoja ajitahidi huu Mradi sasa uishe na
ukabidhiwe ili lengoletu lile na chuo kuweza kudahili Wanafunzi wengi
zaidi Liweze Kufikia”Amesema Ole Nasha..
Mradi
wa Ujenzi wa Chuo cha Ualimu kitangali Unagharimu Shilingi billioni 8
lakini mpaka sasa Wakandarasi wamekwisha Pewa Shilingi Billion 3.2 jambo
ambalo limepelekea Mradi huo Kuchukua Miaka 2 Kushindwa Kumalizika.
Kulia
Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiwa na
Mkuu wa Chuo Cha mafunzo ya Ufundi Stadi VETA Mtwara Samweli Kibehele
wakati wa ziara ya kutembelea Chuo hicho kwa lengo la kutazama mazingira
yanayotumika kufundishia Wanafunzi wa VETA.
Naibu
waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipewa maelezo
ya Mradi wa Ujenzi wa Chuo Cha Ualimu Kitangali na Mshauri wa Ujenzi
Nicodemus Mgaya katika ziara yake ya kutazama Maendeleo ya Ujenzi Huo.
Naibu
waziri wa Elim Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha Akiongea na
wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchii FDC ambacho kimeanzishwa
mwaka 1975 ambacho kinafundisha masomo ya Umeme,Ufundi wa Magari pamoja
na Ushonaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...