Hussein Makame, NEC aliyekuwa Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa
ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mbarouk Salim Mbarouk
ametembelea kata ya Mlowa Bwawani katika Halmashauri ya Wilaya ya
Chamwino mkoani Dodoma kuangalia maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa diwani
wa kata hiyo.
Akizungumza na Wasimamizi wa
Uchaguzi wa kata hiyo na Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Mtera Elizabenth
Gumbo kwa niaba ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mtera, Jaji Mbarouk
ameridhishwa na maandalizi ya Uchaguzi wa kata hiyo.
Jaji Mbarouk amewasisitiza
wasimamizi wa Uchaguzi wa kata hiyo kutumia vipaza sauti kufikisha
ujumbe kwa wananchi kwani njia hiyo itarahisisha kufikisha ujumbe wa
uchaguzi kwa wananchi wengi zaidi wakiwemo wasiojua kusoma na kuandika
badala ya kutegemea zaidi taarifa za mabango.
Akitoa taarifa ya maandalizi ya
Uchaguzi wa kata hiyo kwa niaba ya, Afisa Uchaguzi wa Jimbo hilo
Elizabenth Gumbo alisema maandalizi ya Uchaguzi huo yanakwenda vizuri.Alisema wameshapokea vifaa vya
awali vya Uchaguzi ikiwemo mfano wa karatasi ya kupigia, mabango ya
Uchaguzi, fomu za Uchaguzi, bahasha za karatasi za kura na fedha za
bajeti ya Uchaguzi wa kata hiyo.
Gumbo alisema ameshavitaarifu
vyama vya siasa kuwasilisha orodha ya majina ya mawakala wa vyama vyao
na kwamba wamewaomba wawsilishe na picha za mawakala hao na ratiba ya
kuwaapisha inasubiri muda ambao watakapowasilisha orodha hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC Jaji Mbarouk Salim Mbarouk (kulia) akimueleza jambo Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Mtera mkoani Dodoma, Elizabenth Gumbo (kushoto) wakati alipotembelea kata ya Mlowa Bwawani. Kulia ni Mwanasheria wa NEC, Hamidu Mwanga.
Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Mtera, Elizabenth Gumbo (kushoto) akieleza maandalizi ya Uchaguzi Mdogo wa Udiwani kata ya Mlowa Bwawani kwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mbarouk Salim Mbarouk (katikati).Kulia ni Mwanasheria wa NEC Hamidu Mwanga.
Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Hamidu Mwanga (katikati) akizungumza jambo na Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Mtera mkoani Dodoma, Elizabenth Gumbo nje ya jengo la Halmashauri ya Manispaa ya Chamwino mkaoni Dodoma.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Jaji Mbarouk Salim Mbarouk.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...