Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Internews Tanzania wameendesha mafunzo kwa waandishi wa Habari Kanda ya Kaskazini/Magharibi (Geita, Shinyanga na Simiyu) kuhusu Changamoto za Sheria mpya za habari.

Mafunzo hayo ya siku mbili yaliyoanza Agosti 17,2018 hadi Agosti 18,2018 yanafanyika katika ukumbi wa Alpha Hotel Mjini Geita.

Akifungua Mafunzo hayo,Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Tawi la Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa alisema kupitia mafunzo hayo waandishi wa habari watajengewa uelewa kiuhusu sheria mbalimbali zinazohusu vyombo vya habari na waandishi wa habari na namna waandishi wa habari wanavyoweza kuishi na sheria hizo. 

"Lengo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari na kuangalia changamoto zinazotolewa na sheria hizi sambasamba na kukumbushana miiko ya uandishi wa habari lakini pia kufahamu nafasi ya mwandishi wa habari kama mtetezi wa haki za binadamu",alisema.

Naye Afisa Mradi wa Boresha Habari kupitia Shirika la Internews linalofadhiliwa na USAID Victoria Rowan aliwasihi waandishi wa habari waliopata fursa ya kushiriki mafunzo hayo kutumia vyema elimu wanayopewa. 
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Tawi la Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari mikoa ya Geita Shinyanga na Simiyu kuhusu Sheria za vyombo vya habari katika ukumbi wa Alpha Hotel Mjini Geita - Picha zote na Kadama Malunde & Joel Maduka 
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Tawi la Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akielezea malengo ya semina hiyo 
Afisa Mradi wa Boresha Habari kupitia Shirika la Internews Victoria Rowan akielezea jambo ukumbini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...