MKURUGENZI
mkuu wa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) William Erio amewataka
watumishi wa shirika hilo kufanya kazi kwa bidii na kufikia lengo la
kukusanya Shilingi Trilion 1.5 na kwamba hatovumilia wazembe.
Erio
aliyasema hayo jana katika mkutano wake na Wakurugenzi na Mameneja wa
shirika hilo kwenye ukumbi wa NSSF Ilala Dar es Salaam.
"Mwaka
jana mlipaswa kukusanya shilingi Trillion 1 lakini mlikusanya shilingi
billion 700 pekee hivyo hamkufikia lengo." Mwaka huu katika mpango kazi
ulioidhinishwa na Waziri mnapaswa kukusanya shilingi Trilioni 1.5 target
hii lazima hifikiwe."alisema Erio
Alisema
fedha hizo zitapatikana kupitia uandikishwaji wa wanachama wapya,
makusanya ya fealisema. wanachama wa zamani pamoja na fedha za pango za
majengo ya shirika hilo."Hakuna haja ya kuwa na wanachama lukuki ambao
hawalipi michango yao, ni lazima wafuatiliwe kwa karibu kuhakikisha
michango inalipwa kwa wakati.
"
Najua pia tuna majengo yetu ambayo yapo wazi hayana wapangaji,
nimeshaongea na SSRA wanampango wa kufungua ofisi mikoa yote 26 ya
Tanzania bara, wapange kwenye majengo yetu." alisema.Hata hivyo, Erio
alisema kuwa hatomvumilia mfanyakazi mzembe ambae hatofikia malengo
waliyojiwekea."Mkuu wa idara ambae hatofikia performance tuliyojiwekea
sitomvumilia, naomba target tuliyoiweka ifikiwe, isipofikiwa maana yake
kazi zmewashinda na Mimi sitokuvumilia." alisisitiza.
Erio
alisema kuwa jukumu la kusajili wanachama wote ni la wafanyakazi wote
na si idara moja pekee." Mwaka huu tunatakiwa kuandikisha wanachama
wapya 417,000, NSSF inawafanyakazi 1,000 kila mfanyakazi akileta
wanachama 10 kwa mwezi lazima watalipa michango na tutafikia lengo.
Akisisitiza
hilo alisema malengo ya shirika yalifikiwa kwenye vikao halali vya
wafanyakazi na muktasari ya yatokanavyo kwenye vikao hivyo upo, hivyo ni
jukumu la kila mfanyakazi kutekeleza jukumu lake ili kufikia lengo la
shirika ambalo ni kujiimarisha na kukua zaidi.
Hata
hivyo kwa sasa anaendelea kusoma ripoti mbali mbali za utekelezaji
alizokabidhiwa na mtangulizi wake pamoja na wakurugenzi wa kanda na
kisha atafanya ziara ya kutembelea kila kitengo ili kubaini changamoto
zilizopo miongoni mwa wafanyakazi na kuangalia namna ya kuziondoa.
Erio
ambae awali alikuwa mkurugenzi wa PPF aliteuliwa Julai 14 mwaka huu
kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF akichukua nafasi ya Godius Kahyarara.
Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) William Erio akizungumza na
Wakurugenzi na Mameneja wa shirika hilo kwenye ukumbi wa NSSF Ilala
jijini Dar es Salaam jana huku akiwataka watumishi wa shirika hilo kufanya kazi kwa bidii na kufikia lengo la kukusanya Shilingi Trilion 1.5
Baadhi
ya Wakurugenzi na Mameneja wa shirika la NSSF wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) William Erio ,alipozungumza
nao jana kwenye ukumbi wa NSSF Ilala jijini Dar es Salaam kuhusiana
mikakati mipya ya kuimarisha zaidi mfuko huo,ambapo Watumishi wametakiwa
kufanya kazi kwa bidii na kufikia lengo la kukusanya Shilingi Trilion
1.5 .
Sehemu
ya Viongozi wakuu wa NSSF wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu William Erio ,alipozungumza nao jana kwenye ukumbi wa NSSF
Ilala jijini Dar es Salaam kuhusiana mikakati mipya ya kuimarisha zaidi
mfuko huo,ambapo Watumishi wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kufikia
lengo la kukusanya Shilingi Trilion 1.5 .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...