Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paulo Makonda na Mkuu wa wilaya Kigamboni Sara Msafiri kwenye ukaguzi wa miradi ya maendeleo Kigamboni.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amewataka watendaji wote wa Manispaa za Mkoa wa Dar es salaam kuongeza kasi ya utekelezaji wa Miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao. 

Waziri Jafo ameyasema hayo leo alipokuwa katika ziara ya kikazi kukagua miradi ya maendeleo inayo tekelezwa na serikali katika Manispaa hiyo. 

Katika ziara yake leo ametembelea Manispaa ya Kigamboni na kukagua ujenzi wa Ofisi za Manispaa hiyo pamoja na ujenzi wa Kituo cha afya Kimbiji. 

Katika miradi hiyo, Waziri Jafo hakufurahishwa na kasi ya ujenzi wa Miradi hiyo ya maendeleo huku akiagiza ujenzi wa Ofisi za Manispaa ukamilike kabla mwezi Januari mwaka 2019 ili waondokane na tatizo la kupanga kwenye nyumba ya mtu binafsi. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paulo Makonda amemuahidi Waziri Jafo kwamba wao kama mkoa wamejipanga kutekeleza maagizo yote na kuwataka watumishi wote wa mkoa huo kubadili utendaji kazi wao ili kutekeleza kwa wakati miradi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi mbalimbali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akitoa maelekezo baada ya kukagua miradi ya maendeleo Kigamboni.
Viongozi wakikagua kituo cha Afya Kimbiji.
Viongozi wakikagua ujenzi wa jengo la Ofisi za Manispaa ya Kigamboni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...