Na Frank Mvungi- MAELEZO
Katibu
Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi amewataka Makatibu Wakuu wa
Wizara na Makatibu Tawala wa Mikoa kutekeleza majukumu yao kwa
kuzingatia Sheria , Kanuni, Taratibu na Miongozo inayotolewa na Serikali
ya Awamu ya Tano kila wanapofanya maamuzi.
Akizungumza
leo Jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha siku tatu kwa
Viongozi hao Balozi Kijazi amesema kuwa wanalo jukumu kubwa la
kuhakikisha kuwa wanazingatia taratibu zote ili azma ya kujenga uchumi
wa viwanda ifikiwe kwa wakati na kuwanufaisha wananchi.
“Nafasi
zenu ni za maamuzi hivyo msipofanya maamuzi sahihi na kwa wakati
mtakwamisha shughuli za maendeleo na huduma muhimu kwa wananchi.”
Alisisitiza Mhandisi Kijazi.
Akifafanua,
Mhandisi Kijazi amesema kuwa wajumbe wa mkutano huo wanalojukumu kubwa
la kuhakikisha kuwa wanafanyia kazi masuala yote yatakayoazimiwa katika
kikao kazi hicho cha siku tatu kinacholenga kuongeza tija katika ngazi
ya Wizara na Mikoa kwa kuzingatia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano
yakuleta mageuzi makubwa katika nyanza zote hasa katika huduma
zinazotolewa kwa wananchi.
Aliongeza
kuwa Kikao kazi hicho kina umuhimu mkubwa na kitakuwa kikifanyika kila
mwaka ili kuwapa fursa Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala kubadilishana
uzoefu, kubaini changamoto zilizopo na kuweka utaratibu mzuri wa
kuzitatua kwa maslahi ya wanachi.
Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi akifungua Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
Mtendaji Mkuuwa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja akisistiza jambo wakati wa Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
Sehemu ya Makatibu Wakuu wakifuatilia uwasilisjhaji wa mada mbalimbali kwenye Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Bw. James Syanga akiwasilisha mada kuhusu athari za madawa ya kulevya wakati wa Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
Manaibu Katibu Wakuu na Makatibu Tawala wakifuatilia mada wakati wa Kikao kazi cha Makatibu Wakuu na Makatibu Tawala wa Mikoa kinachofanyika Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Septemba 19, 2018.
Sehemu ya washiriki wa Kikao Kazi cha Makatibu Wakuu wa Wizara na Makatibu Tawala wa Mikoa wakifuatilia kikao kazi chao kinachoendelea Jijijini Dodoma. (Picha zote na Frank Shija- MAELEZO)
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...