Taasisi
ya Dr Ntubayaliwe imepongezwa kwa Kubuni shindano la kutunga hadithi
kwa wanafunzi wa shule za msingi, kitendo kinachosaidia kuibua na kukuza
vipaji vya wanafunzi nchini.
Kaimu
Afisa elimu wa Manispaa ya Kinondoni Mwalimu Martha Kusaga ametoa
pongezi hizo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kutangaza na
kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la Andika Challenge la kutunga
hadithi zenye maana kwa wanafunzi wa shule za msingi za manispaa za
Kinondoni na Ubungo.
Akizungumza
katika hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Dr Ntuyabaliwe Foundation Bi.
Jacquiline Mengi amesema baada ya kuendesha shindano hilo kwa manispaa
mbili za Dar es salaam kwa mafanikio makubwa, sasa shindano hilo
litawashirikisha wanafunzi wa shule za msingi za Tanzania nzima.
Amesema
shindano hilo litadumu kwa miezi mitatu na washiriki wanatakiwa watume
hadithi kupitia sanduku la barua 163, Dar es salaam, huku kila mshiriki
aandike jina lake, jina la shule yake, wilaya na mkoa atokao, na mwisho
wa kuwasilisha hadithi ni mwezi Novemba mwaka huu. Hadithi
zitakazoshinda zitachapishwa kwenye vitabu na kusambazwa katika maktaba
mbalimbali za shule.
Jumla
ya hadithi 1,202 kutoka wanafunzi wa shule za msingi 137 za manispaa za
Kinondoni na Ubungo zilipokelewa na kushindanishwa, ambapo Mshindi wa
kwanza alikuwa Nurath Komba kutoka shule ya msingi Tandale Magharibi.
Nafasi
ya pili ilichukuliwa na Agnes Charles wa shule ya msingi Uzuri, huku
Arsernia Charles akishika nafasi ya tatu, na Zulfa Miraji wa shule ya
msingi Mtangani, na Aisha Hialai wa shule ya msingi Londa wakishika
nafasi za nne na ya tano. Washindi wote na shule wanazotoka
walikabidhiwa zawadi mbalimbali, zikiwemo kununuliwa sare za shule na
vitabu kwa mwaka mzima, kufunguliwa akaunti ya benki.
Kaimu
Afisa elimu wa Manispaa ya Kinondoni Mwalimu Martha Kusaga akizungumza
wakati wa kukabidhi zawadi wa washindi wa shindano la kutunga hadithi
kwa wanafunzi wa shule za msingi lililohisisha wilaya mbili za jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Dr Ntuyabaliwe Foundation Bi. Jacquiline Mengi akitoa
historia ya taasisi ya Dr Ntuyabaliwe pamoja na shindano la shindano la
kutunga hadithi kwa wanafunzi wa shule za msingi lililohisisha wilaya
mbili za jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Afisa elimu wa Manispaa ya Kinondoni Mwalimu Martha Kusaga (kushoto)
akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza kwenye shindano la kutunga hadithi
kwa wanafunzi wa shule za msingi, Nurath Komba kutoka shule ya msingi
Tandale Magharibi. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Dr Ntuyabaliwe
Foundation Bi. Jacquiline Mengi.
Baadhi
ya wanafunzi walioingia kwenye tano bora ya shindano la kutunga hadithi
kwa wanafunzi wa shule za msingi wakipokea zawadi zao zilizodhamniwa na
taasisi ya Dr Ntuyabaliwe lilihusisha wilaya ya Kinondoni na Ubungo.
Meza
kuu ingiongozwa na Kaimu Afisa elimu wa Manispaa ya Kinondoni Mwalimu
Martha Kusaga akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi watano
walioibuka kidedea kwenye shindano la kutunga hadithi kwa wanafunzi wa
shule za msingi lililoshirikisha shule mbalimbali zilizopo kwenye wilaya
mbili za jijini Dar es Salaam.
Walimu
wa shule zilizotoa washindi watano wa shindano la kutunga hadithi kwa
wanafunzi wa shule za msingi wakiwa kwenye picha ya pamoja na meza
kuumara baada ya kukabidhiwa zawadi zao.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...