Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM)
amekabidhi msaada wa Vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 36.5
kwa ajili ya vituo vya afya na zahanati sita zilizopo katika halmashauri
ya wilaya ya Ushetu,Msalala na Kahama Mji wilayani Kahama mkoani
Shinyanga.
Mheshimiwa
Azza amekabidhi vifaa tiba hivyo leo Jumanne Oktoba 16,2018 kwa Mkuu wa
Wilaya ya Kahama,Anamringi Macha wakati wa Kikao cha Baraza la UWT
wilaya ya Kahama uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kahama.
Vifaa
tiba hivyo ni pamoja na shuka 100,mashine za kupima damu,wingi wa
damu,sukari,joto,mapigo ya moyo na vifaa vya kusaidia kujifungua kwa
akina mama ambavyo kupatikana kwake kumetokana na jitihada za mbunge
huyo kuhakikisha vifo vya mama na mtoto vinapungua mkoani Shinyanga.
Awali akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa tiba hivyo,Mheshimiwa Azza Hilal alisema kupitia Kampeni yake ya ‘Afya Yangu Mtaji Wangu’
na kuwajali akina mama aliamua kutafuta wadau kwa ajili ya kusaidia
kumaliza changamoto ya uhaba wa vifaa tiba katika vituo vya afya na
zahanati.
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM)
akizungumza wakati akikabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi
milioni 36.5 kwa ajili ya zanahati na vituo vya afya wilayani Kahama leo
katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kahama.Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kahama,Telephora Saria,kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Myonga.
Vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 36.5 kwa ajili ya zanahati na vituo vya afya wilayani Kahama vilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) kwa kushirikiana na wadau wake Bahari Pharmacy Ltd na Brett &Beileys.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi vifaa tiba kwa Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha.
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi
shuka ikiwa ni sehemu ya shuka 100 alizotoa kwa ajili ya vituo vya afya
na zahanati wilayani Kahama.
Wa
pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akiwa
ameshikilia boksi lenye mashine ya kupimia sukari mwilini. Wa kwanza
kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Myonga.Wa kwanza
kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Ushetu,Mheshimiwa Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi akifuatiwa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiwa ameshikiliwa vifaa tiba.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...