Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa(NIDA) Dkt. Anold Mathias Kihaule, ameenza kazi kwa
kukagua utendaji wa ofisi za Usajili za Mkoa wa Dar-es-salaam ambapo pamoja na
mambo mengine amezungumza na wananchi na kutembelea ofisi ya Serikali ya Mtaa
ambako huduma ya utoaji wa fomu na ugawaji wa Vitambulisho zinaendelea.
Katika ziara hiyo Dkt. Kihaule
aliyekuwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa Mamlaka hiyo; amepongeza kazi
nzuri inayofanywa na wafanyakazi wa NIDA na kusisitiza watumishi kuzingatia
utoaji wa huduma unaozingatia viwango ili kuweza kupunguza malalamiko yasiyo ya
lazima kwa wananchi.
Aidha amewashukuru viongozi na Watendaji
katika Serikali za Mitaa kwa kazi nzuri ya kuwahudumia wananchi kuhakikisha
wanapata Vitambulisho vya Taifa na kuahidi kuendelea kuwapa ushirikiano katika
kuhakikisha malengo ya Serikali yanafikiwa.
Dkt. Anold Mathias Kihaule aliteuliwa
hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo akijaza nafasi iliyoachwa wazi
na Ndg. Andrew W. Massawe aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera, Ajira na Walemavu.
Pichani
ni mmoja wa wakazi wa Kinondoni akimuelezea Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Vitambulish vya Taifa(NIDA), Dkt. Anold Mathias Khaule (wa pili
kushoto) namna alivyopatiwa huduma katika ofisi ya Usajili Wilaya ya
Kinondoni
Mkurugenzi
Mkuu wa NIDA akikagua fomu ya mmoja wa wananchi waliojitokeza
kusajiliwa. Kutoka kulia ni Bw Dickson Mbanga Afisa Usajili wilaya ya
Kinondoni na katikati ni Bw. Alphonce Malibiche, Mkurugenzi wa Idara ya
Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa.
Mkurugenzi
Mkuu NIDA akikagua sehemu ya kutunzia Vitambulisho vya Taifa katika
ofisi ya Usajili wilaya ya Kinondoni. Kuli ni Afisa Usajili wilaya ya
Kinondoni na wa kwanza kushoto ni Bw. Melkiory Ndofi Mkurugenzi wa Idara
ya Fedha na Utawala.
Mkazi
wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Gift Emmanuel Nkya (aliyevaa nguo nyeusi)
mwanafunzi wa mwaka wa kwanza chuo cha Biashara CBE, akizungumza na
Mkurugenzi Mkuu wa NIDA alipotembelea kituo cha Usajili Kawe jijini
Dar-es-salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa NIDA Dkt. Anold Mathias Kihaule akiweka saini katika kitabu cha
wageni ofisi ya Usajili wilaya ya Kinondoni wakati alipofanya ziara
kukagua namna shughuli za Usajili zinavyofanyika kituoni hapo
Mkurugenzi
Mkuu wa NIDA (aliyevaa koti) akiingia kwenye ofisi ya Serikali Mtaa wa
Mzimuni wakati wa ziara yake kukagua uendeshaji shughuli za Usajili
Wilaya ya Kinondoni. Hapa alishuhudia utaratibu wa ugawaji fomu za
Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi na utaratibu wa kugawa
Vitambulisho vya Taifa kupitia ofisi za Watendaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...