Marehemu Ahmed Jongo enzi za uhai wake alipohojiwa na Azam TV
Maziko ya Mtangazaji wa RTD Ahmed Jongo yamefanyika leo makaburi ya Mbagala Charambee Dar
es Salaam
Mtangazaji mkongwe na mmiliki wa redio ya Sports FM Abdallah Idrissa Majura akijumuika na ndugu, Jamaa na marafiki kupata chakula nyumbani kwa marehemu Tandika Maghorofani leo mchana
kwenye mazishi ya aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania
(RTD),Ahmed Jongo
.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa ambaye pia ni Rais Mstaafu wa TFF na mchezaji mkongwe wa Yanga na Taifa Stars Leodegar Chilla Tenga (sahiti la buluu) na aliyewahi kuwa kiongozi wa Yanga Emmanuel Mpangala wakiungana na ndugu, jamaa na marafiki kupa pata chakula cha mchana nyumbani kwa marehemu aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo,nyumbani kwake Tandika Maghorofani,jijini Dar es Salaam.
Waombolezaji wakijadiliana jambo katika msibani wa marehemu aliyekuwa Mtangazaji nguli wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo,nyumbani kwake Tandika Maghorofani,jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni aliyekuwa Meneja wa Uwanja wa Taifa Mzee Frank Macha, mtangazaji Mkongwe Salim Mbonde na mwanasoka guli wa zamani ambaye sasa ni kocha Abdallah King Kibaden.
.
.
Magiwji wa utangazaji nchini toka kulia Abdallah Idrissa Majura, Dunstan Tido Mhando, Salim Mbonde, Ahmed Kipozi na Charles Hilary wakiwa nyumbani kwa marehemu aliyekuwa Mtangazaji maarufu wa Radio Tanzania (RTD),Ahmed Jongo Tandika Maghorofani Dar es Salaam.
Watangazaji, mafundi mitambo wacheza kandanda nyoya wa enzi hizo na viongozi wa soka wakipata picha ya kumbukumbu baada ya kujumuika na ndugu, jamaa na marafiki nyumbani kwa marehemu aliyekuwa Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania (RTD), Ahmed Jongo Tandika Maghorofani,jijini Dar es Salaam.
Kwa Habari zaidi BOFYA HAPA
Kwa Habari zaidi BOFYA HAPA
Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa Amani Mzee Ahmed Jongo.Michuzi Blog asante kwa picha nilikuwa sijawahi kuona picha wala kumuona Salim Mbonde!!TBC Taifa siku moja wawaalike hawa wakongwe watutangazie mechi moja walau dak kumi kumi walau,bado wanaweza.
ReplyDelete