Muandaaji
wa Muziki nchini Tanzania, Producer Pancho Latino almaarufu Mafia ambae
alifanya kazi kwenye studio mbalimbali aliyefariki jana kwa kuzama
kwenye maji kwenye kisiwa cha Mbudya Dar es Salaam anatarajia kuzikwa
Wilayani Gairo, Morogoro.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa na Msanii Fid Q katika ukurasa wake
wa Twitter imesema kuwa Marehemu Pancho Latino itahitimishwa siku ya
Jumamosi nyumbani kwao.
Ibada itaanza saa 4 asubuhi, na baadae wataaga mwili wa marehemu na
maziko yatafanyika saa nane mchana.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Lugalo kwa uchunguzi
zaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...