NA MWAMVUA MWINYI,KIBAMBA.
TAASISI mbalimbali za
kifedha zimeaswa kutoa elimu kwa wajasiriamali kuhusiana na nidhamu ya
matumizi ya fedha katika biashara zao ,kabla ya kuwakopesha ili waweze
kunufaika na mikopo wanayowapatia.
Pamoja na
hayo, wajasiriamali hao wametakiwa kuwa wabunifu kwa kuzalisha bidhaa
zilizo bora na kuhifadhiwa vizuri ili kuendana na soko la ushindani wa
kibiashara.
Hayo yalisemwa na
Beatrice Mbawala ambae alimwakilisha mkuu wa wilaya ya Ubungo jijini Dar
es salaam, wakati wa uzinduzi wa kikundi cha Gogoni Vicoba Investor,
kilichopo kata ya Kibamba .Alieleza, elimu juu
ya fedha wanazokopa wajasiriamali ni muhimu kwani baadhi yao wamekuwa
wakifilisika kutokana na matumizi yasiyo sahihi ya fedha .
Beatrice alisema kuwa
,baadhi ya wajasiriamali wameshindwa kufikia mafanikio na kuwa
wajasiriamali wakubwa kutokana na kushindwa kuwa na nidhamu ya fedha
wanazokopa .“Akinamama
,wajasiriamali mliopo hapa mhakikishe mnakuwa waaminifu na kuwajali
wateja wenu,kuzalisha bidhaa bora na kuacha kutumia mikopo mnayochukua
kutafuta kiki mitaani,kwa kufanya ufahari”alieleza Beatrice.
Nae mkufunzi wa
vicoba kutoka taasisi ya Pamoja Entrepreneurship Support for Community
Development (Pescode) Enethlena Wadelanga alisema ,wanawapa mafunzo ya
ujasiriamali kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi na kifikra na kujitetea
kwa kuunganisha nguvu ujuzi na uzoefu.Alifafanua ,jamii
inapaswa kuamka ili kuleta maendeleo kwa kuungana kwani vita ya kiuchumi
ni ya pamoja kwa ajili ya kuboresha maisha kupitia shughuli zao za kila
siku za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za kila mwanachama.
Enethlena alifafanua,
wanatarajia kujenga ofisi kwa ajili ya kufanyia shughuli zao na
kuanzisha ufugaji wa kuku na kuwaomba wadau kuwaunga mkono hasa taasisi
za kifedha ili waweze kujiinua kiuchumi.Mwanachama Mariam
Kawawa alisema kuwa wangehitaji kutengewa eneo kwa ajili ya
wajasiriamali kufanyia kazi kuliko kila mtu kufanyia sehemu yake ambapo
baadhi ya bidhaa huzalisha uchafua na kutupwa holela.
Mariam alibainisha,
kutokana na kujiunga kwenye vicoba hiyo ameweza kunufaika na mafunzo
mbalimbali ambapo kwa sasa anazalisha bidhaa mbalimbali na kuweza
kujikwamua kiuchumi huku akiwa ametoa ajira kwa watu wengine ambao
anashirikiana nao.Gogoni Investor
ilianzishwa mwaka mmoja uliopita na ina wanachama 50 ambao kuna makundi
mawili A na B ikiwa na malengo ya kujikwamua kiuchumi .
Beatrice Mbawala (wa pili kushoto) akiangalia bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali kutoka kikundi cha Gogoni Vicoba Investor, wakati alipomwakilisha mkuu wa wilaya ya Ubungo jijini Dar es salaam, katika uzinduzi wa kikundi hicho, kilichopo kata ya Kibamba ,(wa kulia) ni mkufunzi wa vicoba kutoka taasisi ya Pamoja Entrepreneurship Support for Community Development (Pescode) Enethlena Wadelanga
Beatrice Mbawala akizungumza wakati alipomwakilisha mkuu wa wilaya ya Ubungo jijini Dar es salaam, katika uzinduzi wa kikundi cha Gogoni Vicoba Investor, kilichopo kata ya Kibamba.Picha na Mwamvua Mwinyi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...