Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mamlaka ya majisafi na majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wamesema kazi ya ujenzi wa mfumo wa usambazaji maji Bagamoyo imekamilika kwa asilimia kubwa maji yamefunguliwa na kufika katika tenki la Bagamoyo.
Kazi ya usafishaji wa mabomba inaendelea kwa ufanisi na inatarajiwa kukamilika leo chini ya usimamizi Mhandisi Lydia Ndibalema Mkurugenzi wa miradi wa Dawasa.na utakapokamilika maji yataanza kwenda tenki la maji la Bagamoyo linalohifadhi Lita Milioni sita kwa siku.
Mradi huo wa Uliojengwa kwa mkopo wa masharti nafuu na unatarajiwa kukamilika rasmi mwezi Desemba mwaka huu na wananchi wa mji wa Bagamoyo watafanikiwa kupata maji. Zoezi hilo la kusafisha mabomba mji wa Bagamoyo utaanza kupata maji kwa wingi na kwa msukumo mzuri kupitia mfumo wa zamani, Mkandarasi wa kujenga na kupanua mfumo mpya wa usambazaji maji anatarajiwa kupatikana wakati wowote.
Mradi huo Oktoba 25 mwaka huu ulitembelewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Hassan Suluhu na kuahidi kufikia Desemba mwaka huu watakuwa wameshaanza kutoa huduma kwa wananchi ikiwa ni moja kati ya mradi wa uboreshaji wa huduma za ugawaji na usambazaji maji katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani.
Mradi huo unaotekelezwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kupitia Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) ulianza rasmi mwezi Machi mwaka 2016 na utakamilika 2018.
Kazi ya mradi huo ipo chini ya mfumo unaohudumiwa na Mtambo wa Ruvu Chini ni pamoja na ujenzi wa matenki tisa ya kuhifadhi na kusambaza maji yenye ukubwa wa kuhifadhi lita Milioni 3.0 hadi 6.0.
Mbali na mradi wa matenki, kuna ujenzi wa vituo vinne vya kusukumia maji, ununuzi wa transfoma na ufungaji wa umeme wa msongo Mkubwa, ununuzi na ulazaji wa mabomba makubwa ya ugawaji maji na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji mitaani yatakayokuwa na urefu wa jumla ya Kilometa zipatazo 80.
Wataalamu wakiwa katika eneo la ujenzi wa mfumo wa usambazaji maji Bagamoyo uliokamilika kwa asilimia kubwa na kufika katika tenko la Bagamoyo linalohifadhi maji lita 6 kwa siku.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...