Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amewataka wataalam wanaopanga maeneo yanayopaswa kupelekewa umeme kupitia miradi mbalimbali kuhakikisha kuwa wanakuwa makini katika upangaji wa maeneo hayo ili kutorundika miradi mingi katika maeneo ambayo tayari yameshasambaziwa umeme.

Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa kikao chake na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati,  Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini ( REA) ambacho kililenga  kupata taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme inayotekelezwa mijini na vijijini.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara ya Nishati, Raphael Nombo ( amemwakilisha Katibu Mkuu), Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Eng. Innocent Luoga, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Eng. Amos Maganga, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka na Kamishna Msaidizi wa Nishati Jadidifu, Edward Ishengoma.

“Kuna maeneo ambayo tayari yana umeme au kuna miradi kadhaa inayotekelezwa katika maeneo hayo hivyo kwa miradi tunayotaka kutekeleza sasa lazima tuweke msisitizo katika maeneo ambayo bado hayajafikiwa na nishati hiyo au hayajasambaziwa umeme kwa kiasi kikubwa,” alisema Dkt Kalemani.

Dkt. Kalemani alitoa kauli hiyo baada Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa REA, Eng. Amos Maganga  kueleza miradi mbalimbali ambayo ipo katika mchakato wa kutekelezwa ukiwemo wa kuongeza wigo wa miundombinu ya usambazaji umeme  (Densification) mzunguko wa pili  katika maeneo mbalimbali nchini na mradi wa usambazaji umeme wa awamu ya Tatu mzunguko wa pili.

Akielezea  kazi ya usambazaji umeme vijijini, Maganga alisema kuwa hadi kufikia Novemba 15, 2018, jumla ya vijiji  4,024  vimepatiwa umeme kupitia miradi ya REA ya Awamu ya Kwanza hadi Awamu ya Tatu mzunguko wa kwanza unaokamilika Juni 2019, mradi wa Makambako- Songea, Mradi wa umeme wa kV 400 wa Iringa hadi Shinyanga,  mradi wa Densification mzunguko wa kwanza na nishati jadidifu.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akiongoza kikao kati yake na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia kwa Waziri) pamoja na watendaji wa Wizara ya Nishati,  Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini ( REA) ambacho kililenga  kupata taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme inayotekelezwa mijini na vijijini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...