BENKI
ya NMB nchini imetoa mabati 229 kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wakima
mama katika hospitali ya wilaya ya Muheza ikiwa ni kuunga mkono juhudi
za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli
kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto za afya kwenye maeneo
yao.
Hafla ya makabidhiano hayo yalifanyika mjini Muheza
na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo akiwemo Katibu wa UWT
Mkoani Tanga Sophia Nkupe na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi
Mwanasha Tumbo.
Akizungumza baada ya kupokea mabati hayo
Katibu wa UWT huyo aliishukuru na kuwapongeza benki ya NMB kwa
kuwakubalia ombi lao la kuwasaidia mabati kwa sababu wamekuiwa mstari
wa mbele kusaidia lakini wanafanya hivyo kuunga mkono juhudui za Rais
katika dhamirta yake ya kuhakikisha huduma za afya zinakuwa bora,.
Nkupe alisema pia wana mpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa
juhudi kubwa anazofanya kuhakikisha wananchi wanaondokana na
changamoto mbalimbali ikiwemo za huduma ya afya na nyenginevyo
“Lakini pia nikushukuru Mh DC Mhandisi Mwanasha Tumbo kwa
juhudi zako unazozifanya kuhakikisha wilaya ya Muheza inapata
maendeleo makubwa pia niwaombe NMB mtusaidie wakina mama kwa sababu
tunateseka sana wanachombezwa na taasisi mbalimbali za mikopo yenye
riba kubwa”Alisema Katibu huyo wa UWT.
Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Cosmas Gabriel kushoto akimkabidhi mabati 229 Katibu wa UWT Mkoani Tanga Sophia Nkupe kwa ajili ya ujenzi wa wodi wakina mama hospitali ya wilaya ya Muheza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
Katibu wa UWT Mkoani Tanga Sophia Nkupe kulia akimkabidhi 229 Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo mabati 229 kwa ajili ya ujenzi wa wodi wakina mama hospitali ya wilaya ya Muheza kushoto ni Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Cosmas Gabriel
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akimkabidhi mabati 229 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza kwa ajili ya ujenzi wa wodi wakina mama hospitali ya wilaya ya Muheza kushoto ni Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kaskazini Cosmas Gabriel
Katibu wa UWT Mkoani Tanga Sophia Nkupe akizungumza katika halfa hiyo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...