Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
MFANYABASHARA Henry  Munisi (30)mkazi wa mkoani Mbeya, Leo Januari 22,2019 amepandishwa katika kizimba  cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo dhidi ya Rais Magufuli.

Akisoma hati ya Mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi Patrick Mwita amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Salum Ally kuwa mshtakiwa ametenda kosa hilo Desemba 28, mwaka 2018 akiwa jijini Mbeya.

Imedaiwa kuwa,  siku ya tukio mshtakiwa Munisi kupitia ukurasa wake wa Facebook  alichapisha taarifa  za uongo zinazosema "Jinsi Magufuli alivyochota Sh.trilioni 1.5 za ATCL akitumia  ujanja wake wa kuleta ndege ili atuibie" huku akijua taarifa  hizo ni za uongo na zina lengo la kupotosha umma. 

Hata hivyo, mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama imemtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho watakaosaini bond ya Sh. 500,000.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka,  upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 6, 2019.

MFANYABASHARA Henry  Munisi (30)mkazi wa mkoani Mbeya, leo Januari 22,2019 akipandishwa katika kizimba  cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu tuhuma za kuchapisha taarifa za uongo dhidi ya Rais Magufuli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...