Meneja wa NMB kanda ya kati Dodoma, Msolo Mlozi amewaomba wananchi wa
Wilaya ya Kiteto, kujiunga na Benki ya NMB kwa kufungua akaunti kwa lengo
la kunufaika na Benki hiyo kwa nyanja mbalimbali zikiwemo Elimu, Afya
na misaada ya Majanga inapojitokeza.
Mlozi ameyasema hayo hivi karibuni akiwa katika Kijiji
cha Chang'ombe alipofika kutoa msaada wa bati, mbao na misumari vya
thamani ya milioni tano, kuondoa adha kwa wanafunzi wa shule ya msingi
Matereka..
Meneja wa NMB kanda ya kati Dodoma, Msolo Mlozi akikabidhi mabati kwa uongozi wa shule ya msingi
Matereka,katika kijiji cha Chang'ombe wilayani Kiteto hivi karibuni.
Meneja wa NMB kanda ya kati Dodoma, Msolo Mlozi akikabidhi mbao kwa Uongozi wa shule ya msingi
Matereka,katika kijiji cha Chang'ombewilayani Kiteto hivi karibuni.
Meneja wa NMB kanda ya kati Dodoma, Msolo Mlozi akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali katika Kijiji cha Chang'ombe alipofika kutoa msaada wa vifaa vya ujenzi kama vile Mabati, Mbao na Misumari vyenye thamani ya shilingi milioni tano, kuondoa adha kwa wanafunzi wa shule ya msingi Matereka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...