Na Said Mwishehe,Globu ya jamii.
VIONGOZI
wa dini mbalimbali nchini wamesema wanaipongeza Serikali ya Awamu ya
Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais Dk.John Magufuli kwa kudhihirisha
namna ambavyo inatambua na kuthamini uwepo wa viongozi wa dini na kuwapa
nafasi.
Wakizungumza leo
Januari 18,2019 wakati wa hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti
Mawasiliano TTMS yaliyofanyika eneo la Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania(TCRA)ambapo mgeni rasmi ni Rais Dk.John Magufuli.
Viongozi
hao wamemwambia Rais Dk.Magufuli kuwa tangu ameingia madarakani
viongozi wa dini wamekuwa wakipewa nafasi kubwa na ya kuheshimiwa na
hivyo wanamshukuru kwa namna ambavyo amewapa nafasi hiyo.Wamesema
kwa nyakati tofauti viongozi wa dini wamekuwa wakijadiliana namna
ambavyo Serikali ya Awamu ya Tano ambavyo imekuwa ikishirikiana kwa
karibu na viongozi hao wa dini.
Sheikh
wa Mkoa wa Dar es Salaam kupitia Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (BAKWATA) Alhad Mussa Salum amesema Rais Magufuli amewapa nafasi
kubwa viongozi wa dini kuliko kipindi chochote kile."Hakika
viongozi wa dini tunayo sababu ya kukiri utawala huu wa Serikali ya
Awamu ya Tano imekuwa karibu nasi,tunashirikishwa kwenye mambo
mbalimbali.
"Hivyo
wamekubaliana kutambua kuwa Serikali ya inayoongozwa na Rais Magufuli
imeamua kuwaweka karibu viongozi wa dini," amesema Sheikh Alhad na
kuongeza viongozi wa dini wataendelea kumuombea yeye na viongozi wengine
wa Serikali na wananchi wote kwa ujumla.
Kwa
upande wake Askofu Mkuu wa Full Gospell Bible Zacharia Kakobe amesema anaungana na
Sheikh Alhad kwa kuelezea kuhusu namna ambavyo viongozi wa dini wanapewa
kipaumbele kwenye Serikali.Amefafanua
Rais Magufuli ameonesha unyenyekevu mbele ya viongozi wa dini na kwake
madhehebu yote ya dini kwake yako sawa,hakuna dhehebu kubwa wala dogo.
"Rais
kabla kuja hapa mbele wakati tumekaa pale tulikuwa tunajadiliana namna
ambavyo umetoa kipaumbele kwa viongozi wa dini.Tunakushukuru kwa uamuzi
wako wa kuwa karibu na viongozi wa dini," amesema Askofu Kakobe.
Kila
viongozi wa dini ambaye alipata nafasi ya kukaribishwa kuomba dua
alitumia nafasi hiyo kuelezea namna ambavyo Rais Magufuli amekuwa na
hofu ya Mungu na amekuwa akimtanguliza Mungu kwa kila jambo na ndio
maana amekuwa akifanikiwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) Zacharia Kakobe katika hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya Ndani na Nje ya Nchi (TTMS) iliyofanyika makao Makuu ya TCRA Jijini Dar es salaam leo Januari 18, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) Zacharia Kakobe katika hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kudhibiti Mawasiliano ya Ndani na Nje ya Nchi (TTMS) iliyofanyika makao Makuu ya TCRA Jijini Dar es salaam leo Januari 18, 2019.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...