WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo wa wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma na ameitaka ifanye kazi kwa weledi.Ameiagiza ifanye marekebisho ya maslahi kulingana na mazingira ya mtumishi, akitolea mfano kada za elimu, afya, kilimo na mifugo ili yalingane na kazi wanazozifanya.
Amekutana na wajumbe wa bodi hiyo leo (Alhamisi,Januari 24, 2019) katika kikao kilichofanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu amesema Serikali ina nia njema ya kuhakikisha mishara na maslahi ya watumishi wa umma nchini yanaboreshwa, hivyo ameiagiza bodi hiyo ifanye kazi kwa bidii.
Amesema Serikali imeunda bodi hiyo ili kupata ushauri utakaotokana na tathmini sahihi ya nini Serikali inatakakiwa kufanya ili kuboresha utendaji wa watumishi wa umma nchini. Serikali inaimani kubwa na wajumbe wote wa bodi hiyo kutokana na uzoefu walionao kwenye utumishi wa umma.
“Tunataka muongozo mzuri wa kuwafanya watumishi wa umma wafanye kazi yao kwa waledi bila ya kuwa na vishawishi vya aina yoyote ikiwemo kuomba na kupokea rushwa.” Amesema Serikali inataka kila mtumishi wa umma anawajibika ipasavyo katika kuwatumikia wananchi mambo ambayo yatakuwa yameimarishwa kutokana na upatikanaji wa maslahi mazuri.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na
Maslahi katika Utumishi wa Umma, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar
es salaam, Januari 24, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi
ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Ummam, kwenye Makazi ya
Waziri Mkuu jiji Dar es salaam, Januari 24, 2019. Kutoka kushoto ni
Mwanasheria wa Bodi, Dkt. Charles Kato, Katibu Msaidizi wa Bodi,
Fortatus Mbiro, Mwenyekiti wa Bodi, Donald Ndagula, Mjumbe wa Bodi,
George Mlawa na Katibu Mtendaji wa Tume, Mariam Mwaniulwa.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya Mishahara na
Maslahi katika Utumishi wa Umma, George Mlawa baada ya mazungumzo na
wajumbe wa Bodi hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam,
Januari 24, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Mwanasheria wa Bodi, Dkt.
Charles Kato, Katibu Msaidizi wa Bodi, Fortatus Mbiro, Mwenyekiti wa
Bodi, Donald Ndagula na Katibu Mtendaji wa Tume, Mariam Mwaniulwa.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...