Na Ripota Wetu
IMEELEZWA kuwa nchi ya Urusi inajipanga kuzima mtandao wa Intaneti kwa muda,
kwa lengo la kujitoa katika mawasiliano na dunia kama sehemu ya majaribio yake ya
kujikinga dhidi ya mashambulio ya kimtandao.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Uingereza ni kwamba mchakato huo utafanya
mawasiliano baina ya raia na mashirika ya Urusi kubaki ndani ya nchi badala ya ya
kupitia njia za kawaida za kimtandao kimataifa.
Tayari rasimu ya Sheria ya kuruhusu mabadiliko ya kiufundi ili kuiwezesha nchi hiyo
kuendesha mtandao wake wenyewe iliwasilishwa bungeni mwaka jana wa 2018 na
kwamba jaribio hilo litafanyika kabla ya Aprili 1 mwaka huu ingawa siku rasmi ya
kuzimwa mtandao haijawekwa wazi itakuwa lini.
Pia inaelezwa kuwa rasimu ya sheria hiyo iliyopewa jina la Programu ya Taifa ya
Uchumi wa Kidijiti, inawataka watoa huduma za intaneti nchini Urusi kuwa na uwezo
wa kuendelea na huduma zao hata pale ikitokea nchi za kigeni zikiamua kuitenga
Urusi.
Wakati hayo yakiendelea nchi wanachama wa NATO na washirika wake wagi Kwa
wamekuwa wakitishia kuiwekea vikwazo vya kimtandao Urusi ambayo wanaituhumu
kwa kufanya mashambulio ya kimtandao.
Hivyo njia mojawapo inayopangwa na Urusi katika kujilinda huko ni kutengeneza
mfumo wake binafsi wa anuani za kimtandao ufahamikao kama DNS, waweze kupata
mawasiliano hata pale watakapotengwa ama kujitenga.
Kwa sasa kuna taasisi 12 zinzoshughulikia suala la utolewaj na matumizi ya anuani
hizo na hakuna hata moja iliyopo Urusi.Hata hivyo tayari kuna chapa nyingi za
mfumo huo wa DNS nchini Urusi hali inayoonesha kuwa nchi hiyo inaweza kuendelea
na shughuli zake za kimtandao hata ikitokea imetengwa leo.
Pia watoa huduma za intaneti wanatarajiwa kuelekeza mawasiliano yote yanayopita
kwao kwenye vituo vya serikali kwenye zoezi hilo. Mawasiliano yote ya ndani ya Urusi
yataruhusiwa kuendelea lakini yale yatokayo nje ya nchi yataminywa.
Kutokana na mkakati huo kunauwezekano wa Serikali ya Urusi itakuwa na ubavu
kama wa China wa kupanga mawasiliano gani raia wake wapate kutoka nje ya nchi.
Hata hivyo vyombo vya habari nchini humo vinadai kuwa watoa huduma za intaneti
nchini humo wanakubaliana na mabadiliko hayo lakini wanatofautiana kwenye
namna gani utekelzwaji wake uwe. Wanaamini jaribio hilo litazaa "mvurugano
mkubwa" kwa matumizi ya mtandao ya nchi hiyo, umeandika mtandao wa ZDNet.
Serikali ya Urusi inawapa fedha watoa huduma ya intaneti nchini humo ili kuboresha
miundombinu yao kuendana na mipango yake ya baadae.Hata hivyo, kuna
uwezekano wa watu kuchupa mazuio hayo ya serikali kwa kutumia mitandao binafsi
(VPNs) - ambayo hudanganya mahala kompyuta ama simu janja ilipo na hivyo
vidhibiti kushindwa kuzizui kupata mawasiliano yaliyokatazwa.
Hata hivyo, baadhi ya nchi kama China zimekuwa wakali kwa wale wanaotumia
tenkolojia hiyo. Ukikutwa unatumia ama kusambaza bila kibali teknolijia hiyo nchini
China unaweza kutupwa jela.
Mara chache, nchi hujikuta zimejitoa kwenye mawasiliano ya intaneti kwa bahati
mabaya - ilitokea hivyo mwaka 2018 nchini Mauritania kwa siku mbili baada ya
nyaya ya chini ya bahari inayopeleka mawasiliano hayo kukatika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...