Na Ripota Wetu
UMOJA wa Afrika umependekeza kufanyika mkutano wa kimataifa Julai mwaka huu
kwa ajili ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa Libya na pia kuitisha uchaguzi Oktoba.
Katika taarifa yake, umoja huo umesema leo Februari 12 ,2019 mkutano huo
utafanyika ili kutafuta maridhiano chini ya uratibu wake pamoja na Umoja wa
Mataifa. Pia umeiomba Tume ya Umoja wa Afrika kushirikiana na Umoja wa Mataifa
na Serikali ya Libya kwa ajili ya kupanga uchaguzi wa urais na bunge mnamo Oktoba
mwaka huu.
Mwenyekiti wa sasa wa Umoja huo, Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amesisitiza
kuwa matatizo ya Afrika yatatatuliwa na waaafrika wenyewe na kwamba Libya
imekuwa chini ya tawala hasimu na makundi ya wanamgambo tangu kuuawa kwa
Moammer Ghadaffi mwaka 2011.
Inaelezwa kuwa uhasama ni baina ya Serikali inayotambulika na jumuiya ya
kimataifa pamoja na ile inayoungwa mkono na Jenerali Khalifa Haftar.
CHANZO: DW
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...