Na Woinde Shizza Globu ya Jamii.
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limetambulisha mfumo mpya wa
ukusanyaji wa Madeni ya Makosa ya usalama barabarani unaotumia kamera
maalumu zenye uwezo wa kupiga picha na kutambua gari linalodaiwa.
Akizungumza na vyombo vya habari mapema leo Kamanda wa jeshi
la Polisi mkoani Arusha Jonathan Shana amesema kuwa mfumo huo mpya
utarahisisha kutambua Magari yote yanayodaiwa kupitia kamera maalumu
zilizofungwa barabarani zitakazo kuwa zikipiga picha na kuonyesha kiasi
ambacho gari linadaiwa.
Kamanda Shana amesema kuwa Jiji la Arusha limepata kamera
tatu za kisasa zinazotembea na zimefungwa katika maeneo mbalimbali
katika Jiji la Arusha na kwamba machine hizo zinauwezo wa kutambua
namba za Magari ya aina mbali mbali.
Mtaalamu wa kitengo cha IT kutoka makao Makuu ya jeshi la
polisi nchini,ACP Mayala Towo amesema mfumo huo umeanza kutumika jijini
dar es salaam tangu mwaka 2015, na sasa unasambaa nchi nzima na lengo ni
kuhakikisha fedha ya serikali zinakusanywa kwa wakati.
Mmoja ya askari wa usalama barabarani anayeendesha mfumo
huo wa kamera, Pc Masalu Yamala amesema zoezi hilo limekuwa na mafanikio
makubwa kwani imerahisisha utambuzi wa Magari yanayodaiwa tofauti na
hapo awali kwa kuwa lilikuwa likipoteza muda mwingi.
kamanda Shana alitumia wasaa huo kujitambulisha kwa
waandishi wa habari na kueleza vipaumbele vyake vya utendaji kazi ikiwa
ni pamoja na kupambana na uingizaji na utumiaji wa Dawa za kulevya
ikiwemo Cocaine, Mirungi na Bangi.7
Picha ikionyesha Mmoja ya askari wa usalama barabarani
anayeendesha mfumo huo wa kamera, Pc Masalu Yamala akiwaonyesha
waandishi Wa habari na wananchi jinsi kamera hiyo inavyofanya
Kazi(Picha na Woinde Shizza globu ya jamii ).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...