MKUU wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru Mkoani
Tanga Christopher Mariba akizungumza na waandishi wa habari ambao
hawapo pichani wakati akitoa taarifa
yao ya miezi mitatu ya utendaji wao ambapo katika kipindi hicho
walifungua shauri moja ambalo lilifikia mwisho na kutolewa maamuzi.
Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali
mkoani Tanga wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Takukuru mkoa wa Tanga
Christopher Mariba wakati akitoa taarifa yao ya miezi mitatu ya
utendaji wao
TAASISI ya kuzuia na Kupamba na Rushwa Mkoani Tanga imemtaka aliyekuwa
mtumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza Idara ya Elimu Aneth
Makame kurejesha kiasi cha milioni 30 alizichukua wakati akijua tayari
amekwisha kustaafu na kuisababishia serikali hasara.
Hayo yalisemwa leo na Mkuu wa Takukuru Mkoani Tanga Christopher Mariba
wakati akitoa taarifa yao ya miezi mitatu ya utendaji wao ambapo
katika kipindi hicho walifungua shauri moja ambalo lilifikia mwisho na
kutolewa maamuzi.
Alisema mtumishi huyo aliomba kustaafu kwa hiyari akiwa na miaka 55
lakini akaendelea kuchukua mshahara kwa miaka mitano iliyofuatia na
hivyo kuisababishia hasara kiasi hicho.
Alisema suala hilo linahusiana na mishahara hewa kutokana na kwamba
baada ya kustaafu kwa hiari mtumishi huyo aliendelea kula mshahara na
kusababisha hasara ya kiasi hicho kwa serikali huku akijua kufanya
hivyo ni kosa kisheria.
Aidha alisema bado mtumishi huyo hajaanza kurejesha fedha hizo huku
taasisi hiyo ikimtaka kufika ofisini kwao yeye na familia yake ili
waweze kuweka utaratibu wa kuzirejesha fedha hizo haraka iwezekanavyo.
“Endapo atashindwa kufanya hivyo basi itabidi tutafute utaratibu
mwengine kupata fedha hiyo nah ii itakuwa ni pamoja na kuuza nyumba au
mali yoyote anayomiliki…kabla ya maamuzi hayo mshtakiwa alikuwa
amekwisha kukaa mahabusu takribani mwaka mmoja na nusu bila
dhamana”Alisema.
Mkuu huyo wa Takukuru Mkoa alisema pia katika kipindi hicho mkoa huu
umeokoa kiasi cha sh.milioni 2,190,500 kilicho kuwa kimechukuliwa
kinyume cha sheria na taratibu za fedha .
“Pamoja na kiasi hicho kurejeshwa tumewaandikia barua waajiri wa
wahusika kwa lengo la kuweza kuchukua hatua za kinidhamu /kiutawala
dhidi ya watumishi waliohusika na matendo hayo “Alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...