Na woinde shizza globu ya jamii Arusha
Wanariadha
nyota wa Tanzania Alfonce Simbu na Josephy Panga ni miongoni mwa
wakimbiaji mashuhuri ambao watashiriki katika mashindano ya Ngorongoro
marathon yanayotarajiwa kufanyika April 20 mwaka huu.
Wakimbiaji
wengine nyota waliothibitisha kushiriki mashindano ni pamoja na Failuna
Matanga,Anjelina Tsere ,Magdalena Shauri ,Fabian Joseph ,Faraja Damas
pamoja na Natalia Elsante.
Akizungumza
na Globbu ya Jamii leo muandaaji wa mbio hizo Meta Petro alisema kuwa mbio hizi
ambazo zinafanyika kwa miaka 12 mfululizo zitashirikisha wakimbiaji
zaidi ya 1000 kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo wakimbiaji mashuhuri
kutoka nchini Kenya.
Alisema
mbio hizo zitakuwa za kilometa 21 ,kilometa tano pamoja na kilometa
mbili na nusu kwa ajili ya watoto ambapo alitaja zawadi kuwa mshindi wa
kwanza wa kilometa 21 atapata milioni moja ,mshindi wa pili atapata
laki tano ,na mshindi wa tatu atapewa laki tatu.
Alitaja malengo ya mbio hizo ni kupiga vita ujangili pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani.
"Unajua
wananchi wengi na maanisha wa Tanzania wengi wamekuwa na tabia ya
kutotembelea hifadhi zetu za taifa hivyo mbio hizi zitasaidia
kuhamasisha wa Tanzania kuwa na tabia ya kutembelea hifadhi zetu"
alisema Meta
Alisema
kuwa kwa washindi wa mita zote ambao watashika kuanzia Namba tano hadi
kumi wao watapata fursa ya kutembelea mbuga ya wanyama ya Ngorongoro
kwa ajili ya kujionea vivutio vilivyopo katika hifadhi hiyo.
Alitoa wito kwa wa Tanzania kujitokeza kushiriki mbio hizo .
Muandaaji wa Ngorongoro marathon akizungumza na Mwandishi wa habari hizi hii leo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...