Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa hoteli ya Mount Meru wakati wa kuwakaribisha Wanahisa wa Benki ya CRDB katika Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa ishirini na nne utakaofanyika siku ya jumamosi tarehe 18 Mei, 2019, katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha. Mkutano huo utatanguliwa na Semina ya Wanahisa itakayofanyika ijumaa tarehe 17 Mei 2019. Kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Joseph Witts.
Baadhi ya wageni wakifatilia mkutano kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela na waandishi wa habari, uliofanyika mapema leo kwenye hoteli ya Mount Meru, jijini Arusha.
Benki ya CRDB kufanya Mkutano Mkuu wa ishirini na nne wa Wanahisa tarehe Mei 18, 2019. Akizungumza na Wandishi wa Habari katika hoteli ya Mount Meru iliyopo Jijini Arusha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Ndugu Abdulmajid Nsekela amesema Mkutano huo wa Wanahisa wa Benki ya CRDB utafanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC uliopo katika Jijini hilo la Arusha.

“Kama ilivyo ada Benki ya CRDB imeandaa Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa Benki unaotarajia kufanyika tarehe 18/05/2019”, alisema Ndugu Nsekela.

Nsekela alisema Mkutano huo wa Wanahisa wa Benki ya CRDB utatanguliwa na Semina maalum kwa Wanahisa itakayofanyika tarehe 17/05/2019 katika ukumbi huo huo wa AICC ambapo Mgeni rasmi atakuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kasim Majaliwa Majaliwa. Ndugu Nsekela amesema katika Semina hiyo Wanahisa wa Benki ya CRDB watapata kufahamu juu ya fursa mbalimbali zinazopatikana kwa kuwa sehemu ya Wanahisa wa Benki.

Akiwahamasisha Wanahisa wa Benki wa Benki ya CRDB kuhudhuria katika Mkutano Mkuu, Ndugu Nsekela alisema kuhudhuria kwao ni muhimu sana kwani kunaisaidia Benki katika kupanga na kuidhinisha mikakati mbalimbali endelevu itakayoiwezesha Benki ya CRDB kufanikisha malengo iliyojiwekea na hivyo kuendelea kutengeneza faida kwa Wanahisa.

Akizungumzia kuhusu agenda za mkutano huo wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, Ndugu Nsekela alisema ni pamoja na kupitisha na kusaini kumbukumbu za Mkutano Mkuu wa Mwaka wa ishirini na tatu uliofanyika tarehe 19 Mei 2018, kupokea na kupitisha Taarifa za Fedha na ripoti za Wakurugenzi kwa mwaka ulioishia tarehe 31 Desemba 2018, kuidhinisha taarifa maalumu ya gawio kwa mwaka ulioishia tarehe 31 Desemba 2018, kuchagua wajumbe wapya wa Bodi, kuidhinisha uchaguzi wa wakaguzi wa hesabu wanaokubalika kisheria kwa mwaka unaoishia tarehe 31 Desemba 2019, kupanga mahali na tarehe ya Mkutano Mkuu ujao pamoja na kujadili mapendekezo mbalimbali kutoka kwa Wanahisa wa Benki juu ya uboresha wa huduma za Benki.

Nsekela alimalizia kwa kuwahamasisha Wanahisa wa Benki ya CRDB kuhudhuria kwa wingi katika mkutano huo mkuu wa Wanahisa wa Benki YA CRDB, “Naomba nichukue fursa hii tena kuwakaribisha Wanahisa wote wa Benki ya CRDB katika Mkutano Mkuu kwani kuhudhuria kwao ndio mafanikio ya mkutano huo.

Kwa Mwanahisa ambaye hawataweza kuhudhuria yeye mwenyewe ana haki yakuchagua mwakilishi au wawakilishi kuhudhuria na kupiga kura kwa niaba yake”, alisema Ndugu Nsekela.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...