MSHAMBULIAJI na nyota wa klabu ya Yanga sc Heritier Makambo inasemekana kuna tetezi za sintofahamu kuwa ametimkia nchini Guinea ambapo amesaini kandarasi ya miaka 3 na klabu ya Horoya Athletic inayocheza ligi kuu nchini humo kwa ada ya 230,000,000 za kitanzania.
Kwa mujibu wa ukurasa wa Instagram wa Yanga umesema kuwa Makambo mwenye umri wa miaka 25 amesaini mkataba wa kuitumikia klabu hiyo miaka 3 na kupewa nafasi kubwa ya kufanya makubwa kwenye ligi kuu ya nchi hiyo hasa baada ya kuonyesha mafanikio makubwa akiwa kwenye kikosi cha Yanga.
Makambo aliebakiza mkataba mmoja wa kuitumikia Yanga uliokuwa umalizike mwakani 2020.
Hata hivyo mwenyekiti wa klabu ya Yanga Mshindo Msolla ameweka wazi kwa taarifa hizo zinazoleta sintofahamu kwa kueleza kuwa mshambuliaji huyo aliondoka na kocha Mwinyi Zahera Mwinyi nchini Guinea kuonana na uongozi wa timu hiyo kwa ajili ya kufanya vipimo vya afya na ambapo angefaulu vipimo hivyo alipaswa kurudi nchini kuja kufanya mazungumzo na uongozi.
"Ni kweli Makambo aliondoka juzi na mwalimu Zahera kuelekea nchini humo kwa ajili ya vipimo vya afya kwa klabu ya Horoya, hivyo basi tunawasubiri warudi tuitazame ofa yao kisha tufanye biashara"amesema Mwenyekiti huyo.
Aidha Msolla amesisitiza kuwa "hizo taarifa za kutambulishwa rasmi sizielewi ila mwalimu akirudi tutatizama ofa yao na kulingana na klabu nyingine nyingi zinazomtaka mchezaji huyo kisha tufanye maamuzi"
Nyota huyoa ambaye ni raia wa Congo alisajiliwa na klabu ya Yanga ya Tanzania akitokea Fc Lupopo ya nchi kwao kwa dau lisilopungua milioni 60 za kitanzanzania.
Mshabuliaji Herieter Makambo akiwa katika uzi wa Horoya Athletic klabu ya Guinea na viongozi wa timu hiyo amabapo inasemekana ameshasaini mkataba wa miaka 3 na klabu hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...