Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (katikati)
akizungumza na wazalishaji wa mifuko mbadala wa plastiki (hawapo pichani).
Katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam,
pamoja na mambo mengine wazalishaji hao wa mifuko mbadala wameihakikishia
Serikali kuwa wako tayari kuongeza kasi ya usambazaji wa mifuko mbadala kote
nchini. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira Nchini Dkt. Samuel Gwamaka. Kulia Dkt. Freddy Manyika Kaimu Mkurugenz
Idara ya Mazingira.
Sehemu ya wazalishaji wa
mifuko mbdala wa plastiki kutoka Kampuni mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba (hayupo
pichani) katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam, pamoja na
mambo mengine wazalishaji hao wa mifuko mbadala wameihakikishia Serikali kuwa
wako tayari kuongeza kasi ya usambazaji wa mifuko mbadala kote nchini ikiwa ni
utekelezaji wa agizo la Serikali la kusitisha matumizi ya mifuko ya plastiki
hapa nchini ifikapo tarehe 1 Juni 2019.
Bw. Heneriko Batamuzi kutoka
Kampuni ya Kenwood Enterprise (T) Ltd akichangia mada katika kikao cha wadau
cha kupitia Rasimu ya Kanuni za
kusimamia Taka Hatarishi hapa nchini. Ofisi ya Makamu wa Rais imeandaa rasimu
ya Kanuni mpya za kusimamia Taka Hatarishi nchini ikiwa ni pamoja na ukusanyaji,
urejelezaji, uteketezaji na usafirishaji wake ndani na nje ya nchi. Kikao hiki
kimefanyika katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...