Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba
John Kabudi amesaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Vietnam
hapa nchini kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Rais wa Taifa hilo Jenerali
Le Duc Anh aliyefariki April 22,2019.
Akizungumza
mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi huo wa
Vietnam Profesa Palamagamba John Kabudi ametoa pole kwa wananchi wa
Vietnam na kuongeza kuwa Jamhuri ya Kisoshalisti ya watu wa Vietnam na
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zina uhusiano wa muda mrefu na wa miaka
mingi tangu enzi za Jamhuri ya watu wa Vietnam wakipigania Uhuru wao
kutoka kwa Mareakani na Ufaransa.
Ameongeza
kuwa Uhusiano baina ya Jamhuri ya watu wa Vietnam na Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa sasa umekuwa katika nyanja ya kiuchumi hususani
katika eneo la mawasiliano ambapo ameitaja kampuni Halo tell kama
mojawapo ya kampuni iliyowekeza katika sekta ya mawasiliano.
Ameyataja
mahusiano mengine yapo katika sekta ya kilimo hususani katika kilimo
cha korosho na kahawa na kwasababu hizo kama mataifa Rafiki ya muda
mrefu amefika katika ubalozi huo kwa ajili ya kuhani msiba wa aliyewahi
kuwa Rais wa Taifa hilo Jenerali Le Duc Anh ambaye amefariki akiwa na
umri wa miaka 98.
Kwa
upande wake Balozi wa Jamhuri ya watu wa Vietnam hapa nchini Balozi
Nguyen Kim Doanh,amshukuru Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi kwa kufika kwake kuhani
msiba huo na kuongeza kuwa hali hiyo inaendelea kukuza na kuimarisha
ushirikiano uliopo baina ya mataifa hayo mawili.
Amemtaja
Jenerali Le Duc Anh kama mmoja wa viongozi waliokuza kwa kiasi kikubwa
mahusiano baina ya Tanzania na Vietnam na kwamba ana matumaini makubwa
kwa siku za usoni mahusiano baina ya nchi hizi mbili yataendelea kukuzwa
na kuimarishwa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiweka saini katika kitabu cha maombolezo cha ubalozi wa Vietnam hapa nchini kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Rais wa Taifa hilo Jenerali Le Duc Anh aliyefariki April 22,2019, wa pili kutoka kushoto ni Balozi wa Vietnam hapa nchini Mhe. Nguyen Doanh na watatu kutoka kulia ni Mke wa Balozi Doanh pamoja na maafasia ubalozi huo wakishuhudia tukio hilo. Mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo Prof. Palamagamba John Kabudi ametoa pole kwa wananchi kupitia kwa Balozi wa Vietnam hapa nchini nakuelezea kuwa Jamhuri ya Kisoshalisti ya watu wa Vietnam na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zina uhusiano wa muda mrefu na wa miaka mingi tangu enzi za Jamhuri ya watu wa Vietnam wakipigania Uhuru wao kutoka kwa Mareakani na Ufaransa.

Profesa Palamagamba John Kabudi akizungumza na Balozi Doanh
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...