Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imeshiriki maonesho ya kimataifa ya Biashara ya 43 kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam ili kuonesha huduma mbalimbali zinazotolewa na Bodi hiyo pamoja na utoaji wa elimu kwa wananchi waliofika kwenye banda la Bodi hiyo lililo ndani ya jengo la Wizara ya Fedha na Mipango.

Baadhi ya huduma zinazotolewa na NBAA katika kipindi hiki cha Sabasaba ni Usajili wa Wanafunzi ili kuweza kufanya mitihani ya Bodi hiyo kwa ngazi mbalimbali  kuanzia ngazi ya chini (Accounting Technician)  mpaka  ile ya Taaluma (Profession) pamoja na usajili wa wanachama  na makampuni ya kihasibu na Kikaguzi. 

 Pia Bodi itaanzisha mfumo wa kidijitari wa kutoa huduma zake hususan usajili wa wanafunzi na Wananchama kupitia tovuti yao.

Afisa Masoko na Mawasiliano kutoka Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Magreth Kageya(kulia) akitoa ufafanuzi wa kazi mbalimbali zinazotolewa na Bodi hiyo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya kimataifa ya Biashara ya 43 yanayofanyika kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James akizungumza jambo alipotembelea banda la Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwenye maonesho ya kimataifa ya Biashara ya 43 yanayofanyika kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la NBAA kwenye maonesho ya kimataifa ya Biashara ya 43 yanayofanyika kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James akiagana na maafisa wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Evelyn Mcharo(kushoto)  na Magreth Kageya(wa pili kushoto) kwenye maonesho ya kimataifa ya Biashara ya 43 yanayofanyika kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...