Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula leo amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Vietnam, ukiongozwa na Makamu Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ndugu Trinh Dinh Dung, katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yao, walijikita zaidi katika mahusiano baina ya Chama Cha Mapinduzi na Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam na Serikali zinazoongozwa na vyama hivyo.
"Kwa kweli Sisi CCM na Serikali yake tunaridhirika na kufurahia sana jinsi Chama Cha Kimomunisti na Serikali yake ya Vietnam vinavyotupa ushirikiano katika masuala mbalimbali ya kisiasa na kimaendeleo", alisema Mangula.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula akimkaribisha Makamu Waziri Mkuu wa Vietnam Ndugu Trinh Dinh Dungkwa katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula akimpa zawadi Makamu Waziri Mkuu wa Vietnam Ndugu Trinh Dinh Dungkwa kabla ya kufanya mazungumzo na Ujumbe wake katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula akipokea zawadi kutoka Makamu Waziri Mkuu wa Vietnam Ndugu Trinh Dinh Dungkwa kabla ya kufanya mazungumzo na Ujumbe wake katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula katika mazungumzo na Makamu Waziri Mkuu wa Vietnam Ndugu Trinh Dinh Dungkwa na Ujumbe wake katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula akiwa na Makamu Waziri Mkuu wa Vietnam Ndugu Trinh Dinh Dungkwa baada ya kufanya mazungumzo na Ujumbe wake katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndugu Philip Mangula katika picha ya pamoja na Makamu Waziri Mkuu wa Vietnam Ndugu Trinh Dinh Dungkwa na Ujumbe wake katika Ofisi Ndogo ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...