Na Editha Karlo,wa michuzi Tv,Kigoma

JESHI la wananchi wa Tanzania(JWTZ) limesema kuwa litawaadhibu wale wote watakaojaribu kuvuruga amani na usalama wa nchi na limetoa tahadhari kwa watu wote wanaotumia mapori vibaya kuacha kufanya hivyo mara moja.

Mkuu wa Brigedi ya kanda ya magharibi (202 Kikundi cha Vikosi) Brigedia Jenerali, Julius Mkunda alisema hayo mkoani Kigoma wakati akiahirisha zoezi la kijeshi la kujiweka tayari kwa wapiganaji wa jeshi kupambana adui pindi anapotokea na kusema kuwa amani na usalama wa Watanzania ni lazime upewe kiupaumbele.

katika zoezi hilo lililofanyika kwenye mapori ya wilaya za Kibondo, Kasulu na Kakonko na kutambulika kama kama Opereshini KIKAKA Brigedia Jenerali Mkunda alisema kuwa kumekuwa na uharibifu mkubwa wa mapori hayo, kutumika kwa shughuli za maficho ya ujambazaji, uwindaji haramu na kilimo mambo ambayo yanafanywa na wageni kutoka nchi jirani.

"Tanzania siyo shamba la bibi kwa kila anayetaka anakuja kufanya anachojisikia, hatutakubali tutawaadhibu wale wote wenye nia mbaya ya kutumia mapori yetu kwa vitendo ambavyo ni kinyume cha sheria na taratibu za nchi yetu, lakini vinatishia amani na usalama wa raia na mali zao na kuwafanya waishi kwa woga,"Alisema Brigedia Jenerali Mkunda.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Mkuu wa mafunzo na utendaji kivita kutoka Brigedi ya kanda ya Magharibi, Kanali Wilbert Ibuge alisema kuwa mapori yote ambayo watu wanayaona nchini yana wenyewe na wenyewe ni jeshi la wananchi wa Tanzania ambao wana wajibu wa kuyatunza na kuyalinda na hivyo hakuna mtu yeyote ambaye ataingia kwenye mapori hayo akaachwa ayatumie anavyotaka.

Mkuu huyo wa mafunzo alisema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya utimamu na utayari wa jeshi kujindaa kupambana pindi adui anapotokea na kwa sababu kwenye vita hakuna mahali pa kufanya majaribio hivyo kazi ya kuwasaka na kuwakamata wale wote ambao wataingia kwenye mapori hayo na kufanya vitendo vya uhalifu itatumika kama sehemu ya mazoezi kwa vitendo kwa wapiganaji.

Mkuu wa kikosi cha 24 KJ mkoa kigoma ambacho kimesimamia na kuratibu mafunzo hayo, Meja J.S.Luhonyva akisoma risala kuhusu mafunzo hayo alisema kuwa mazoezi hayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa na vijana wameonyesha kuwa tayari kukabiliana na adui pindi atakapotokea.
Meja Luhonvya alisema kuwa lengo la mazoezi hayo kwa kiasi kikubwa limefikiwa ambapo medani zote za mapambano kivita zimefanyika na vijana wapiganaji wameonyesha wako tayari wakati wowote watakapotumwa kwenda mstari wa mbele kulinda nchi yao.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa kigoma,Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga Mkuu wa wilaya Kasulu, Kanali Simon Hanange alisema kuwa zoezi hilo kwao kama mkoa ni hatua kubwa kuelekea katika kuhakikisha kwamba mkoa unakuwa na amani na usalama lakini mapori yote yanatumika kwa manufaa ya Taifa badala ya watu wachache kwa maslahi yao.
Mkuu wa Brigedia ya magharibi 202KV Julius Mkunda akisoma risala yake wakati akihairisha zoezi la kujiweka tayari lililotambulika kama operesheni KIKAKA kwa wapiganaji wa jeshi pindi anapotokea adui.
Askari wakishangilia kwa morali baada ya zoezi walilokuwa wanafanya la kujiweka tayari kupambana na adui au oparesheni kikaka kufungwa leo
Askari wakiwa wanamsikiliza Mkuu.wa Brigedi ya kanda ya magharibi 202 KV Brigedia Jenerali Julius Mkunda (hayupo pichani)wakati akihairisha mafunzo ya oparesheni kikukuu yaliyofanyika kwa siku 14 kwa Wilaya za Kakoko,Kasulu na Kibondo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...