Na Karama Kenyunko, 

WANAWAKE wawili, Magdalena Uhwello na Halima Nsubuga wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka saba yakiwemo ya kuendesha biashara ya upatu na utakatishaji fedha.

Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kati ya Aprili Mosi, 2017 na Juni 30, 2017 washitakiwa walikula njama ya kutenda kosa la kusimamia na kuendesha biashara ya upatu.

Katika shtaka la pili imedaiwa, tarehe na mahali hapo, washitakiwa walikusanya fedha kutoka kwa watu mbali mali ambazo walikuwa wakichangia kwa kuwaahidi kuwapatia faida watakayopata.

Washtakiwa hao pia wanadaiwa kujihusisha na muamala wa USD 394,265 kwenye akaunti ya Magdalena na Halima kupitia Benki ya Equity Tanzania Ltd wakati wakijua kwamba fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la kuendesha biashara ya upatu.

Inadaiwa Aprili 22, 2017 maeneo ya jiji la Dar es Salaam, washtakiwa kwa lengo la kuficha chanzo halali cha fedha hizo, walihamisha USD 12,309 kwa Benki ya Equity Uganda kwa jina la Smart Magara.

Pia Aprili 24,2017 washitakiwa hao wanadaiwa kuhamisha USD 29,890 kwenye akaunti ya jina hilo.

Aliendelea kudai Aprili 25,2017 maeneo ya jiji la Dar es Salaam washitakiwa hao walihamisha USD 58,743 kupitia benki hiyo ya Equity Uganda.

Pia inadaiwa Aprili 21,2017 washitakiwa walihamisha USD 83,718 kwenye benki ya Equity Uganda kwa jina la Magara huku wakijua kwamba fedha hizo ni zao la makosa ya kuendesha biashara ya upatu.Hata hivyo, wshitakiwa wamekana kutenda makosa hayo na kwa mujibu wa sheria mashitaka wanayoshitakiwa nayo washitakiwa hao hayana dhamana

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.Wakili wa utetezi, Peter Kibatala anayewatetea washtakiw aliomba mahakama kupanga tarehe fupi kwa ajili ya kutoa hoja za kisheria kuhusu uhalali wa hati ya mashitaka.

Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 30, mwaka huu kwa ajili yakutajwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...