NA VICTOR MASANGU, PWANI
WAWEKEZAJI wa sekta ya viwanda wametakiwa kuhakikisha wanazingatia
sheria na taratibu zote za kazi na kuachana na vitendo vya kuvunja
sheria za nchi kwa kuamua kuwanyanyasa wafanyakazi wao kwa kuwanyima
haki zao za msingi ikiwemo kuwapatia huduma ya matibabu, pamoja na
kuwapatia maslahi yao kama inavyotakiwa bila ya kuwa na vitisho
vyovyote ili kutumiza azma ya serikali ya kuwa na uchumi wa kati
ifikapo mwaka 2025.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist
Ndikilo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja kwa ajili ya
uwekeji wa jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengenezea vifungashio
(WANDE PRINTING) vitumikavyo katika sekta ya chakula,kilimo,viwanda,
afya, ujenzi pamoja na viwanda ambacho kinajengwa katika eneo la
kata ya Pangani Wilayani Kibaha na kuwaasa watendaji na mamlaka
zinazohusika kuwapa ushirikiano wa kutosha wawekezaji hao bila ya
ubaguzi na ubinafsi wowote.
Ndikilo alisema kwamba serikali ya awamu ya tano lengo lake kubwa ni
kuendelea kushirikiana bega kwa wawekezaji mbali mbali wa ndani na nje
ya nchi kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Rais Dk Jojn Pombe
,Magufuli hivyo wafanyakazi wanatakiwa kupewa haki zao stahiki bila ya
kuonewa hasa katika suala la vitendea kazi pindi wanapokuwa katika
utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
“Katika Mkoa wa Pwani kwanza nashukuru kwa sasa tunaendelea
kushirikiana na wawekezaji wazawa ambao wamekuwa na nia ya kuendelea
kuwekeza katika sekta ya viwanda katika maeneo mbali mbali. Lakini
kila siku Rai yangu kubwa ni kuwapa haki zao zote waafanyakazi kwani
wao ndio wapo mstari wa mbele katika kuzalisha bidhaa, kwa hivyo
katika hili naomba sana kwa wawekezaji kuliangalia kwa jicho la
tatu.”alisema Ndikilo.
Aidha Mkuu huyo aliipongeza Benki ya Azania kwa kuweza kuonyesha
uzalendo kwa kushirikiana bega kwa bega na serikali ya awamu ya tano
katika kuwapa sapoti na kuwawezesha mikopo wawekezaji ikiwemo kiwanda
hicho kwa lengo la kuweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa
wananchi kupitia sekta ya viwanda.
Kwa upande wake mmoja wa wawekezaji wazawa katika kiwanda hicho John
Obach akisoma risala kwa mgeni rasmi kwa niaba viongozi wenzake
amebainisha kuwa ujenzi wa mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi
bilioni 6.6 na kwamba wanatarajia kutoa ajira zaidi ya 300 ambazo
zitaweza kuwasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi na kuondokana na
wimbi la umasikini.
Naye Mkurugenzi wa Azania Benki Charles Itembe ambao ndio
wamewezesha kwa kiasi kikubwa ujenzi wa mradi huo wa kiwanda amesema
kwamba lengo lao kubwa ni kuunga mkono sera ya Rais wa awamu ya tano
Dr. John Pombe Magufuli ya kuwa na uchumi wa viwanda na kuahidi
kuendelea kushirikiana na wawekezaji wengine katika kuinua sekta ya
viwanda.
“Sisi kama taasisi ya kifedha Azania Benki nia na madhubmuni yetu
makubwa ni kuhakikisha tunaaunga sera ya Rais wetu wa awamu ya tano Dk
, John Pombe Magufuli katika kuwa na Tanzania ya viwanda, kwa hivyo
ndio maana tumeamua kuwawezesha wenzetu wa kiwanda hiki cha
kutengenezea vifungashio ili kuleta mapinduzi ya kuwa na uchumi wa
kati ifikapo mwaka 2025.
Pia liongeza kwa sasa wataendelea kutoa sapoti kwa wadau wa maendeleo
pamoja na serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata fursa mbali
mbali za ajira kupitia miradi ya ujenzi ywa viwanda ambavyo vinajengwa
katika maeneo tofauti lengo ikiwa ni kuondokana na wimbi la umasikini
na jukikwamua kiuchumi.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wa kulia akipeana mkono na Mwenyekiti wa makampuni ya Global Packaging na Wande Printing Joseph Wasonga mara baada ya kumalizika kwa zoezi la uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengenezea vifungashio kilichojengwa Wilayani Kibaha.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akikagua moja ya bidhaa ambazo zinazalishwa katika kiwanda cha Wande Printing ambacho kinatengeneza vifungashio wakati alipofanya ziara yake ya kikazi kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kuwanda hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarit Ndikilo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali, viongozi wa kiwanda hicho pamoja na wadau mbali mbali wa maendeleo ikiwemo Mkurugenzi wa benki ya Azania kulia kwake Charles Itembe.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akisalimiana na viongozi mbali mbali wa serikali ambao walifika kwa ajili ya kushuhudia halfa ya uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda hicho cha vifungashio.
Mwenekano wa moja ya mitambo iliyopo katika kiwanda cha kutengeenzea vifungashio ambacho kinatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni Wilayani Kibaha.
Mwenyekiti wa makampuni ya Global Packaging na Wande Printing Joseph Wasonga akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani juu ya mwenendo mzima katika uzalishaji wa kiwanda hicho cha kutengenezea vifungashio.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akisalimiana
na Mwenyekiti wa makampuni ya Global Packaging na Wande Printing
Joseph Wasonga mara baada ya kutoa neno la utambulisho katika halfa
hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...