Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya jeshi ussu wakionyesha uwezo wao wa kupanga risasi ndani ya dakika mbili kwenye maonesho yaliyofanyika mbele ya Mhe.Waziri wa utalii na maliasili.
Gwaride la wahitimu wa mafunzo ya jeshi ussu wakipita mbele ya Waziri wa utalii na maliasili katika sherehe hizo.
Gwaride la wahitimu wa mafunzo ya jeshi ussu wakipita mbele ya Waziri wa utalii na maliasili katika sherehe hizo.
Mmoja
wa wahitimu wa mafunzo ya awali ya jeshi ussu akipita juu ya kamba
katika moja ya maonesho yaliyofanyika mbele ya waziri wa utalii na
maliasili Mhe.Khamis Kigwangaka katika sherehe ya kuhitimisha mafunzo
hayo
Na Jusline Marco-Arusha
Waziri
wa maliasili na utalii Dkt.Khamis Kigwangala ametoa siku 14 kwa manaibu
katibu wakuu na katibu mkuu wa wizara hiyo kuwasilisha mchakato wa
mswada wa sheria ya uundwaji Jeshi Ussu ofisini kwake ili iweze
kuwasilisha bungeni.
Ametoa
agizo hilo katika sherehe za kuhitimisha mafunzo ya Awali ya Jeshi Ussu
katika kituo cha mafunzo cha Mbulu-mbulu kilichopo katika kata ya Kambi
ya simba,Wilayani Karatu Mkoani Arusha.
Dkt.Kigwangala
amesema kuwa kutokukamilika kwa mswada huo ni mapungufu ya wizara kwani
amekuwa akielekeza mara kadhaa mswada huo ukamilike na umekuwa
haukamilishwi.
"Katika
maagizo niliyopewa na Mhe.Rais sikusudii kujiona nikitumbuliwa
kwasababu ya kuchelewa kutimiza wajibu wangu,"Alisema Dkt.Kigwangala
huku akiongeza kuwa kama ni madokezo ameandika mara kadhaa lakini
wamekuwa wakijivuta.
Ameongeza
kuwa kwa zaidi ya miaka kumi tangu ilipoelekezwa na sheria ya uhifadhi
ya wanyamapori haijawahi kuanza ila kwasasa taasisi mbalimbali za
uhifadhi wa wanyamapori zimeanza kuonyesha bidii katika kuwapatia
mafunzo wafanyakazi wao kwenye eneo la Jeshi Ussu.
Vilevile
ametoa jukumu kwa bodi ya mamlaka ya uhifadhi wa wanyamapori Ngorongoro
kupeleka ushauri wa mapendekezo yaliyotolewa ya kufanya kiwtuo hicho
kuwa kamili kwa kuangalia vigezo vyote vitakavyowezesha kufanya kituo
hicho kuwa kituo cha kudumu.
Awali
akitoa risala yake kwa mgeni rasmi mkuu wa kutuo hicho Kanali Martin
kilugha amesema kuwa jumla ya wahitimu wa mafunzo hayo ni 112 ambapo
katika mafunzo hayo wakufunzi wa ndani wametumika,wakufunzi wa hifadhi
pamoja na wakufunzi wa muda kutoka katika jeshi la JWTZ kwa ajili ya
kuimarisha Jeshi Ussu.
Amesema
kuwa wahitimu hao wamefundishwa mafunzo mbalimbali ya uhifadhi ikiwemo
utimamu wa mwili,na ulinzi wa nadharia na vitendo na kufaulu kwa
madaraja mbalimbali.
Kwa
upande wake mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo amesema kuwa
kumekuwa na matukio mengi ya ujangili ya kuuawa kwa wanyama hivyo
wahitimu wa mafunzo hayo wanapaswa kufahamu kuwa wanajukumu kubwa la
kuhakikisha wanalinda rasilimali za nchi.
"Niwaomba
wahitimu walio chini ya uongozi wako Mhe.Waziri wakapambane na ujangili
ili kukomesha mchezo huo na rasilimali za nchi ziweze kuwa salama kwa
faida ya wananchi kwani huo ndio msimamo wa Rais wetu ndiyo maana
ameridhia tuende kwenye mfumo wa kijeshi kama sehemu yake ya kuonyesha
dhamira ya kupambana na ujangili na kulinda rasilimali zetu".Amesema
Mkuu huyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...