Afisa
Mauzo wa Kampuni ya Kansai Plascon (T) Ltd, FloraMapunda,akimkabidhi
mfano wa hundi Mshindi, Robson Majura, mshindi wa Promosheni ya Nunua na
ushinde Rangi za Plascon .Mshindi alikabidhiwa fedha tasilimu kiasi cha
shilingi,!1,000,000,(milioni moja) jana katika Ofisi za Kampuni hiyo
Barabara ya Nyerere Jijini Dares Salaam.
Muwakilishi
kutoka kampuni ya Plascon Mkoani Mwanza Subodh Issar akimkabidhi Frank
Silver mshindi wa Promosheni ya Nunua na ushinde Rangi za Plascon
.Mshindi alikabidhiwa fedha tasilimu kiasi cha shilingi
1000,000,(milioni moja) jana katika Ofisi za Kampuni Jijini Mwanza.
Washindi kujishindia zawadi za pesa taslimu
Dar
es Salaam: Promosheni ya Paka Rangi ya Plascon na Ushinde imerejea, na
sasa inakuja na toleo maalumu la rangi, maarufu kama Rangi ya Pesa kwa
nia njema ili kuwanifaisha wateja wake. Mwaka huu washindi watajishindia
na zawadi za pesa taslimu.
Hayo
yalisemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Hussein Jamal,
alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo kipya cha
mauzo ya rangi ya Plascon, jijini Dar es Salaam.
Jamal
alisema, “Kibiashara tunafurahi kuwa na kampeni kama hii ambapo kupitia
katika promosheni yetu , tuna uhakika kwamba, kuwapo na ushindi wa pesa
taslimu kutaleta nyuso za furaha kwa washindi katika kipindi chote cha
msimu wa kampeni hii.
Promosheni
ya Paka Rangi na Ushinde inatupatia fursa, siyo tu kuwazadia wateja
wetu muhimu, watumiaji wa rangi na wauzaji, lakini pia kujenga msingi wa
mafanikio ambayo tumeyapata kupitia bidhaa yetu ya hii ya Plascon,
tangu tulipoizindua mwaka 2017,”
Kadhalika,
Jamal alifafanua kuwa, promosheni hiyo ni ushahidi tosha wa kuonesha
jinsi ambavyo Plascon imeamua kutoa huduma kwa watanzania na namna
biashara yake inavyolenga kuongeza thamani katika uzalishaji wa rangi
bora, zenye viwango, utafiti na wenye lengo la kukidhi haja ya mahitaji
ya rangi na kutoa ushauri bora kwa watanzania na watumiaji wa rangi kwa
ujumla.
Promosheni
iliyopewa jina la ‘Colour of Money’ itaendeshwa kuanzia Otoba 7 hadi
Desemba 14, 2019, na inatarajia kushirikisha mamia na maelfu huku kila
mshiriki akiwa na uhakika wa kutotoka mikono mitupu .
Meneja
Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo, Tyron Immelmann, alisema kuwa, mwaka
huu , Plascon itatoa zawadi za pesa taslimu shilingi milioni tano kila
wiki, ambapo kila siku kutakuwa na mshindi wa Sh 1,000,000 taslimu.
Washiriki
watatakiwa kununua lita 20 za rangi ya Plascon, na kupewa kadi ambayo
mteja ataisugua na na kutuma namba zake za bahati kwenda 15054, baada ya
hapo atakuwa katika nafasi nzuri ya kuibuka mshindi.
Matangazo
ya Msimu huu wa Promosheni ya Paka Rangi Ushinde na Rangi ya Pesa,
yatatangazwa kupitia vipeperushi kutoka kwa wauzaji, halikadhalika
kupitia katika radio na televisheni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...