Na Said Said Mwishehe,Michuzi Globu ya jamii

KAMPUNI ya Teknolojia ya malipo ulimwenguni(VISA) imezindua kampeni katika msimu huu wa sikukuu Watanzania wenye kadi ya  VISA wataweza kufanya malipo yao ya manunuzi bila kutumia fedha taslimu ambapo pia watakaofanya manunuzi watapata zawadi mbalimbali .

Kampeni hiyo imezinduliwa jijini Dar es Salaam na Kampuni ya VISA imewahimiza wanunuaji bidhaa katika Jiji hilo kwenda katika maduka makubwa kwa ajili ya kufanya manunuzi katika msimu huu wa sikukuu.

Akizungumza kuhusu kampeni hiyo, Meneja wa VISA nchini Tanzania Olever Njoroge amesema itaendelea hadi Desemba 22 mwaka huu ambapo wateja ambao watafanya malipo kwa kutumia kadi ya VISA na VISA kwenye simu ya mkononi  watapata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali.

Amesema kampeni hiyo ambayo wameizundua kwa ajili ya wateja wenye Kadi za VISA ina malengo  ya kuhamasisha utumiaji wa kadi ya VISA au VISA kwenye simu wakati wa manunuzi katika maduka ya Mliman City Mall, Shoppers Masaki na Shopers Mikochoni.

"Kampeni hii ina malengo ya kukuza utumiaji wa kadi ya VISA na VISA kwenye simu ya mkononi, Tunawahamiza wateja wetu wa Tanzania kufanya malipo kwa njia ya Visa ambapo itawapa urahisi na usalama kipindi cha manunuzi wakati huu wa Krismasi,"amesema Njoroge.

Ameongeza kuwa wanaileta VISA kwa Watanzania wakizingatia faida katika kufanya manunuzi yao kwa kutumia kadi ya VISA au VISA kwenye simu ya mkononi ma kwamba wanajivua kwamba sasa Watanzania wapo huru kutumia njia mpya za malipo bila kuwa na fedha mkononi.

Amefafanua kuwa kampeni hiyo ya Krismasi na VISA itawapa wanunuzi  fursa ya kuchagua Zawadi za aina gani kumpatia mteja wao kwa njia rahisi na salama wanaponunua bidhaa kwenye Mall.

Amesema mapema mwaka huu VISA kwa kushirikiana na benki 15 za Tanzania wazilizindua VISA kwa njia ya simu ya mkononi ."VISA kwa kushirikiana kwa njia ya simu ya mkononi ni suluhisho la malipo ya dijiti ambayo inaruhusu watumiaji kutumia fedha kwa kila mmoja bila kulipa ada ya ununuzi. 

"Kutumia huduma hiyo ,mtu anapaswa kupakua app ya benki yake, atafute VISA kwenye app na alipe  bidhaa na huduma kwa kuiscan code ya QR au kwa kutumia nambari ya USSD,"amesema huku akielezea wazi Watanzania wengi wamekuwa na muamko mkubwa wa kutumia VISA kufanya malipo katika manunuzi mbalimbali.
 Mfanyakazi wa Kampuni ya VISA Mary Njau (kushoto) akiwa na moja ya wateja wanatumia VISA kufanya malipo wakati wa uzinduzi wa kampeni inayoitwa  'Sherekea na Visa' ambayo imezinduliwa jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...