NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
INAELEZWA
kuwa kati ya wilaya zinazoongoza kwa maambukizi makubwa ya VVU mkoani
Pwani ni Kibaha Mjini ikifuatiwa na Mkuranga na Chalinze.
Akizungumza
kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Pwani, katika maadhimisho ya siku ya
Ukimwi kimkoa ,huko Mwendapole ,Kibaha Mji,katibu tawala wa mkoa
,Theresia Mmbando aliwataka wakuu wa wilaya kushirikiana na wananchi
kuweka mikakati na vipaombele ili kudhibiti maambukizi mapya ya VVU.
Aidha
,alisema mkoa huo unakabiliwa na baadhi ya changamoto zinazokwamisha
juhudi za mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi ikiwemo kukosekana kwa
mashine ya kupima wingi wa virusi vya Ukimwi ,biashara ya ngono,vigodoro
na idadi ndogo ya vituo vya kutolea huduma ya kufubaisha VVU.
Theresia
alibainisha ,pia ipo changamoto ya mila potofu katika jamii,ndoa za
utotoni,maegesho ya malori,uzinzi,baadhi ya wana ndoa kutokuwa waaminifu
na watu wanaojidunga madawa ya kulevya.
Hata hivyo alisema,hadi kufikia 2017, takwimu za kiwango cha maambukizi ni 5.5. Theresia
alieleza licha ya hayo maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi miongoni
mwa wanaume,wanawake na vijana ,vijana wenye umri kati ya miaka 15-49 ni
mkubwa.
"Mwaka huu
Januari -Oktoba maambukizi kwa wanaume yalikuwa 2,944 kati ya wanaume
133,832 waliopima maambukizi ya VVU sawa na asilimia 2.3."
"Kwa
wanawake yalikuwa ni 5,145 kati ya wanawake 187,222 waliopima
maambukizi ya VVU sawa na asilimia 2.7 na kwa upande wa vijana kuanzia
miaka 15-24 maambukizi mapya ni 1,020 kati ya 95,559 waliopima sawa na
asilimia 1.1"alieleza Theresia.
Nae mratibu wa masuala ya Ukimwi ,Kibaha Mjini Siwema Cheru alisema ,halmashauri hiyo inahamasisha
jamii kuendelea kupata ushauri nasaha na kupima VVU na kwa wale
wanaogundulika na maambukizi ya VVU kupata ushauri na kuanzishiwa dawa
za kufubaza VVU .
Siwema
alifafanua ,pia kuhamasisha WAVIU kujiunga kwenye vikundi ili
kurahisisha utoaji huduma na hadi sasa kuna vikundi 17 vya watu
wanaoishi na Ukimwi na VVU.
Kwa upande wake ,makamu mwenyekiti wa KONGA ,Kibaha Mjini,Antonia Mango,aliomba
kupitia serikali za mitaa (TAMISEMI) itoe tamko kwenye halmashauri
kutenga asilimia fedha za shughuli za UKIMWI kama ilivyofanya kutenga
asilimia 10 kwa ajili ya vikundi vya wanawake,vijana na walemavu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...