Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga akikata utepe kuashiria kupokea rasmi mtambo uliotolewa na Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa Chuo cha Ujenzi Morogoro (MWTI) wakati wa hafla ya kuupokea mtambo huo iliyofanyika chuoni hapo. Katikati ni Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Japhet Y. Maselle na kulia ni Mkuu wa chuo hiko Mhandisi Melkizedeck L. Mlyapatali. Pamoja na mtambo huo pia wamekabidhiwa kompyuta kwa ajili ya shughuli za kimasomo.
Pichani ni mtambo pamoja na kompyuta zilizogaiwa kwa Chuo cha Ujenzi Morogoro (MWTI). Mtambo huo umetolewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katika hafla iliyofanyika chuoni hapo ambapo mgeni rasmi alikua Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle, Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi Mhandisi Lazaro Vazuri pamoja na Mkuu wa Chuo cha Ujenzi Morogoro (MWTI) Mhandisi Melkizedeck L. Mlyapatali wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa chuo hiko mara baada ya kumaliza hafla ya kukabidhi mtambo pamoja na kompyuta kwa chuo hiko iliyofanyika mjini chuoni hapo mjini Morogoro.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga akifurahia mara baada ya kuuupokea rasmi mtambo ambao Chuo cha Ujenzi Morogoro (MWTI) kimekabidhiwa mapema leo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle katika hafla iliyofanyika chuoni hapo. Pamoja na mtambo huo pia wamekabidhiwa kompyuta kwa ajili ya shughuli za kimasomo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle kulia aliyeshika kipaza sauti akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mtambo kwa Chuo cha Ujenzi Morogoro (MWTI) iliyofanyika chuoni hapo, mtambo huo utatumika kufundishia wanafunzi kwa vitendo pamoja na kuingizia kipato chuo hiko kwa kufanya shughuli za ukodishaji. Mbele yake ni Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...