NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO
WATU
zaidi ya 25,319 wamejitokeza kujiandikisha na wengine kuweka kumbukumbu
zao sahihi ,katika zoezi la kuboresha daftari la kudumu la wapiga
kura,wilayani Bagamoyo ,mkoani Pwani.
Aidha
,katika zoezi hilo kulijitokeza changamoto ndogo ndogo upande wa
mashine za BVR ,lakini ushirikiano ulikuwepo katika kutatua changamoto
zinapojitokeza kupitia wataalamu mbalimbali wa TEHAMA na kutoka Tume ya
Taifa ya uchaguzi .
Akitoa
taarifa hiyo, wakati wa baraza la madiwani ,Halmashauri ya wilaya ya
Bagamoyo ,mwenyekiti wa halmashauri hiyo Ally Ally Issa alisema, vituo
vilivyopo wilayani hapo ni 126 ambapo hakuna changamoto kubwa
iliyoripotiwa kukwamisha zoezi tangu lianze .
Aliwahamasisha
vijana waliofikia umri wa miaka 18 mwaka huu ,wasipuuzie zoezi hili
,wajitokeze kwa wingi ili kupata fursa ya kumpigia kura kwakuwa ni haki
ya msingi.
"Ukifikia siku
ya nne ya zoezi wamejitokeza watu 25,319, nawasihi walengwa waendelee
kujitokeza kwa wingi,waliohama eneo moja hadi jingine, waliopoteza
vitambulisho vyao, waliofikisha miaka 18,"
"
,Lengo kubwa halina kificho ,tujitokeze ili kupeleka kura za kishindo
kwa Rais John Magufuli ,hakuna haja ya kupindisha maneno maana hakuna
asiyeona kama Tanzania imepiga hatua kubwa kiuchumi na kimaendeleo ndani
ya miaka mitano ya uongozi wake, Kura zisiwe za kuzitafuta Rais
Magufuli apigiwe kura za kutosha ili aendeleze jahazi"aliongeza Ally .
Nae
katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bagamoyo, Salum Mtelela alitoa wito
hususan kwa vijana kuacha kufanya ajizi katika fursa hiyo adhimu ili
kuweza kumpigia kura Rais, mbunge na diwani katika maeneo yao husika.
Alisema, pasipo kuwa na kichinjio ni kazi bure hivyo walengwa wajitokeze ili kutimiza haki yao ya msingi ya kupiga kura.
"Tunataka
kura za sunami kwa mwenyekiti wetu Taifa wa CCM ,wabunge na madiwani,
maana wembe ni ule ule kama uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na
vitongoji,CCM iibuke kidedea ,hivyo kama kichinjio ukiwa huna utapunguza
kura "alihamasisha Mtelela.
Wakazi
wa Bagamoyo, waliojitokeza kuweka kumbukumbu zao kwenye zoezi hilo,
Riziki Kadiri, Abdul Ally na Martha Thomas walisema ,zoezi hilo halina
kero ya foleni ,wala vipingamizi ndio maana limefanikiwa tofauti na
vitambulisho vya Taifa-NIDA.
Riziki
alisema ,awali alikuwa akiishi Matipwili na sasa kahamia Bagamoyo
,kutokana na kuhama kata amekwenda kujiandikisha katika kata anayoishi
sasa ili aweze kumpigia kura Rais,diwani na mbunge.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...