TAARIFA RASMI YA SERIKALI KUHUSIANA NA
KUREGEZA BAADHI YA MASHARTI KATIKA KUKABILIANA NA MRIPUKO WA COVID-19
ZANZIBAR, TAREHE 27 MEI, 2020
NDUGU WANANCHI,
KWANZA KABISA HATUNA BUDI KUMSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA
KUTUJAALIA UZIMA NA AFYA NJEMA NA KUWEZA KUTIMIZA MOJA KATI YA NGUZO ZA
KIISLAMU YA KUFUNGA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI, KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA IDDI
EL-FITRI PAMOJA NA KUINGIA KATIKA MWEZI WA SHAWAL NA KWA WALE WANAOENDELEA NA
FUNGA YA SITA NAWATAKIA FUNGA NJEMA.
NDUGU WANANCHI,
BAADA
YA SERIKIALI KUFANIKIWA KUKABILIANA KWA KIASI KIKUBWA NA MRIPUKO WA COVID – 19,
SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR INACHUKUA UAMUZI WA KUREGEZA BAADHI YA MAMBO
TULIYOKUWA TUMEAMUA HAPO AWALI KAMA IFUATAVYO:-
1. SERIKALI
YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR INAUNGANA NA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA KUHAKIKISHA KUWA KUANZIA TAREHE
01 JUNI, 2020 VYUO VYOTE VYA ELIMU YA JUU VITAFUNGULIWA NA KUENDELEA NA
PROGRAMAU ZAO KAMA KAWAIDA KWA UPANDE WA ZANZIBAR
2. WANAFUNZI
WA KIDATO CHA SITA NAO WATAANZA MASOMO YAO TAREHE
01 JUNI, 2020 ILI KUWAWEZESHA KUFANYA MITIHANI YAO YA TAIFA. KUFUATIA
MAAMUZI HAYA SERIKALI IMEIAGIZA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI
KUSHIRIKIANA KIKAMILIFU NA WIZARA YA AFYA KATIKA KUANDAA MIONGOZO YA KIAFYA
ITAKAYOPASWA KUZINGATIWA ILI KUEPUKA MAAMBUKIZO YA MARADHI HAYA.
3. KWA
WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA HADI CHA TANO PAMOJA NA WANAFUNZI WA SKULI ZA
MSINGI, MAANDALIZI NA MADRASA, SKULI NA VYUO VYAO ZITAENDELEA KUFUNGWA HADI
YATAKAPOTOLEWA MAELEKEZO MENGINE YA SERIKALI.
4. KWA
UPANDE WA MICHEZO, LIGI KUU YA MPIRA WA MIGUU ZANZIBAR ITAENDELEA KUANZIA TAREHE 5 JUNI, 2020 NA TUMEIAGIZA
WIZARA YA VIJANA, UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO KWA KUSHIRIKIANA NA ZFF PAMOJA NA
WIZARA YA AFYA KUANDAA MUONGOZO NA NAMNA BORA YA KUENDESHA LIGI HIYO.
5. KWA
UPANDE WA MICHEZO MENGINE YOTE INAYOCHEZWA NA VILABU AU VIKUNDI AU MAKUNDI YA
WANANCHI NA MTU MMOJA MMOJA IKIWEMO MAZOEZI, MASHINDANO YA VIWANJANI NA
UFUKWENI YOTE YATASUBIRI HADI ITAKAPOTOLEWA TAARIFA NYENGINE HAPO BAADAE.
NDUGU WANANCHI,
TOKEA
UGONJWA WA CORONA KURIPOTIWA RASMI HAPA ZANZIBAR TAREHE 18 MACHI, 2020 SERIKALI IMEKUWA IKIFUATILIA KWA KARIBU
MWENENDO WA UGONJWA HUO NA HADI KUFIKIA LEO JUMLA YA WAGONJWA 134 WAMETHIBITISHWA KUWA NA MARADHI
HAYO, KATI YAO WAGONJWA 109
WAMEPATIKANA UNGUJA NA 25 PEMBA,
WAGONJWA 6 KWA BAHATI MBAYA
WAMEFARIKI DUNIA TUNAMUOMBA MWENYEZI MUNGU AWASAMEHE MAKOSA YAO NA AWALAZE
MAHALI PEMA PEPONI - AMIN.
NDUGU WANANCHI,
JUMLA
YA WAGONJWA 115 WAMEPONA NA WAGONJWA
19 TU NDIO WANAOENDELEA NA MATIBABU KATIKA KAMBI ZA MATIBABU UNGUJA NA PEMBA, KATI
YA HAO, WAGONJWA KUMI (10) WAPO
HOSPITALI YA KIDONGO CHEKUNDU, WATATU
(3) WAPO SKULI YA SEKONDARI YA JKU MTONI, WAWILI (2) WAPO KIHINANI NA MMOJA
YUPO KATIKA KITUO CHA KIDIMNI UNGUJA. KWA UPANDE WA PEMBA KUNA WAGONJWA WATATU AMBO WAPO KATIKA KITUO CHA
VITONGOJI. WAGONJWA WOTE HAO WANAENDELA VUZURI NA MATIBABU NA AFYA ZAO
ZINAENDELEA KUIMARIKA.
NDUGU WANANCHI,
JITIHADA
HIZO ZOTE ZIMEFANIKIWA KUTOKANA NA UTEKELEZAJI WA MAELEKEZO NA MAIGIZO YA
VIONGOZI WETU WAKUU WA KITAIFA AKIWEMO RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MHE. DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI NA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA
LA MAPINDUZI MHE. DKT ALI MOHAMED SHEIN, NICHUKUE NAFASI HII KUWAPONGEZA KWA
DHATI VIOGOZI WETU HAO NA TUNAAHIDI KUENDELEA KUFUATA KIKAMILIFU MAELEKEZO YAO
KATIKA KUKABILIANA NA MARADHI HAYA.
NICHUKUE
PIA FURSA HII KUWASHUKURU KWA DHATI WANANCHI KWA JINSI AMBAVYO WAMEKUWA WATIIFU
NA WASIKIVU KWA KUFUATA MAELEKEZO NA USHAURI UNAOTOLEWA NA VIONGOZI WETU PAMOJA
NA WATAALAM WA AFYA.
NDUGU WANANCHI,
PAMOJA
NA SERIKALI KUREGEZA MASHARTI YALIYOTOLEWA YA KUKABILIANA NA MARADHI HAYA
INASISITIZWA KWA WANANCHI KUWA BADO MARADHI HAYA YAPO NA NI TISHIO
YANAYOENDELEA KUIATHIRI DUNIA. HATA HIVYO, BAADA YA UZOEFU TULIOKWISHA UPATA
WANANCHI SOTE HATUNA BUDI KUPUNGUZA HOFU NA BADALA YAKE SOTE TUENDELEE KUCHUKUA
TAHADHARI STAHIKI ZA KINGA NA MASHARTI YANAYOENDELEA KUTOLEWA NA WATAALAM WA
AFYA.
ZANZIBAR BILA YA KORONA INAWEZEKANA
AHSANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA!
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...