Na Pamela Mollel,Arusha.
Chuo cha uhasibu Arusha (IAA) kimeendelea kutoa mafunzo ya biashara kwa vikundi vya wafugaji, wakulima na wasindikaji katika Kipindi cha nanenane Arusha, ambapo wanawajengea uwezo ili waweze kufanya shughuli zao kwa tija zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Chuo cha uhasibu Arusha,Prof Eliamani Sedokeya amesema kuwa pamoja na Mambo mengine chuo hicho kinaendelea kutoa mafunzo kwa vikundi mbalimbali ili waweze kumudu soko vizuri
Pia amesema Chuo hicho kinaendelea kufanya udahili kwa wanafunzi wa kozi mbalimbali zinazipatika chuoni hapo katika ngazi za Astashahada,Stashahada na Shahada ya uzamili
Ametaka wanafunzi na wadau wa elimu kuchangamkia fursa hiyo ya kuendelea kujiunga na chuo hicho yenye matawi yake Arusha,Babati na Dar es Saalam
Kauli mbiu ya mwaka huu ni "kwa maendeleo ya kilimo,mifugo uvuvi chagua kiongozi bora 2020"
Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha,Prof Eliamani Sedokeya akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya nane nane katika viwanja vya Taso Mkoani Arusha
Mhadhiri wa chuo cha uhasibu Arusha Felix Mlay akitoa mafunzo kwa vikundi mbalimbali vya ujasiriamali
Afisa Udahili Mr. Gerald Malisa akitoa elimu kwa makundi ya watu waliotembelea banda hilo
Baada ya kupata mafunzo vikundi mbalimbali vilipatiwa vyeti
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...