Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akiongea na baadhi ya wazee waliofika katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga na kujadiliana nao kuhusu masuala mabalimbali yahusuyo wazee hao.Baadhi ya wazee wa Mkoa wa Shinyanga wakisikiliza hoja mbalimbali za viongozi wa mkoa wa Shinyanga jana mkoani Shinyanga.
MKUU wa mkoa wa Shinyanga Dkt Philemon Sengati amehaidi kulifanyia kazi suala la wazee wanaotelekezwa na watoto wao kwa kuitisha vikao vya familia kwa lengo la kuzitaka familia hizo kubeba jukumu la kutunza wazee lakini pia kurejesha mahusiano yao.
Dkt. Sengati alitoa ahadi hiyo baada ya baadhi ya wazee wa Mkao wa Shinyanga kudai kuwa baadhi yao wametekelezwa na watoto wao na wengine kuachiwa kulea wajukuu na watoto wao ambao wana nguvu za kutosha kuwatunza watoto pamoja na wazee.
Dkt. Sengati alisema hayo jana alipofanya kikao cha pamoja na wazee wa mkoa wa Shinyanga ikiwa ni hatua yake muhimu ya kukutana na kusikiliza makundi tofauti ya jamii katika Mkoa wa Shinyanga.
Adha Dkt. Sengati aliwambia wazee hao kuwa ataendelea kuimarisha mabaraza ya wazee mkoani humo kwani baadhi ya mabaraza hayo hayafanyi kazi vizuri na kuziagiza Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga kufanyia kazi changamoto za kibajeti ili wazee hao waweze pia kupata mikopo ya Halmashauri kama ilivyo kwa makundi mengine.
‘’Tutaendelea kushughulikia changamoto za kibajeti hasa ile asilimia mbili ambayo huwa ni lazima itengwe kutoka mapato ya ndani kwa lengo la kuwahudumia wazee kama kundi maalum lakini imekuwa haiwekwi na kwa namna moja au nyingine mmekuwa hamuipati.’’Aliongeza kiongozi huyo wa Mkoa wa Shinyanga.
Aidha Dkt. Sengati ametaka kila mwana Shinyanga kujielimisha lakini pia kutoa elimu kuhusu mira na desturi na imani potofu ya mahuaji ya wazee na kuwa na mtazamo chanya kwa kundi hili la wananchi hodari.
Katika hatua nyingine Dkt. Sengati alizitika Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga kuendelea kuelemisha wazee hao namna bora ya kupata mikopo kutoka katika Taasisi za fedha na Halmashauri ili wazee waweze kijihimarisha kiuchumi na kuchangia katika Maendeleo ya Taifa.
Naye Mzee Mohamedi Mkambala mkazi wa Manispaa ya Shinyanga alimwambia Mkuu wa Mkoa kusaidia wazee katika suala zima la kimatibabu kwani wazee hao mara kwa mara wamekuwa wakiandikiwa madawa ambayo yamekuwa hayapatikani hospitalini.
‘’Kuhusu suala la Afya wazee wanapewa dawa za bure lakini wamekuwa wakiandikiwa kwenda kununua dawa izo hela watapata wapi wakati wana andikiwa dawa za bure?Alihoji Mzee Mkambala.
Katika madai tofauti tofauti ya wazee hao Bi. Judithi Kalwalala aliangazia suala la usalama na kuomba msaada wa Jeshi la Polisi kuingilia kati kwani vibaka wamekuwa wakivamia nyumba zao wakiwa wamevalia madera na kuwabia mali zao huku wakijua hakuna wanaume wakuwalinda.
Dkt. Sengati jana alifanya kikao cha pamoja na wazee wa mkoa wa Shinyanga ikiwa ni hatua yake muhimu ya kukutana na kusikiliza makundi tofauti ya jamii na atakutana na makundi mengine kama hayo kwa lengo la kuona namna bora kufanyia kazi matatizo ya wananchi mkoani Shinyanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...