Na Karama Kenyunko Michuzi TV

WAFANYABIASHARA Abdallah Chande, mkazi wa Tegeta Ununio na Crispin Francis anayeishi Ununio Tegeta, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya zenye uzito wa zaidi ya kilo saba.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Ester Martin mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Evodia Kyaruzi imedaiwa Juni 10,2021 huko Kimara Kilungure katika Manispaa ya Ubungo mkoani Dar es Salaam, washtakiwa wakutwa wakisafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine zenye uzito wa kilo 7. Na gramu 73.

Aidha mshtakiwa Francis anadaiwa siku hiyo akiwa eneo la Kinondoni Manyanya alipatikana akisafirsha dawa za kulevya aina ya bangi zenye uzito wa gramu 2.94.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Julia 8,mwaka huu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...