Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango akimkabidhi zawadi ya mchoro wa Picha ya wanyama watano wakubwa (Big Five) wanaopatikana nchini Tanzania waziri anaeshughulikia masuala ya Biashara ya Kimataifa na Uchumi  Mhe. Franck Riester Paris Nchini Ufaransa Julai 2, 2021.


Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika mazungumzo na waziri anaeshughulikia masuala ya Biashara ya Kimataifa na Uchumi Mhe. Franck Riester Paris Nchini Ufaransa Julai 2, 2021.Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango akimkabidhi zawadi ya mchoro wa Picha ya wanyama watano wakubwa (Big Five) wanaopatikana nchini Tanzania waziri anaeshughulikia masuala ya Biashara ya Kimataifa na Uchumi Mhe. Franck Riester Paris Nchini Ufaransa Julai 2, 2021.

**************************

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na waziri anaeshughulikia masuala ya Biashara ya Kimataifa na Uchumi Mhe. Franck Riester Paris Nchini Ufaransa hii leo Julai 2, 2021.

Katika mazungumzo yao, pande zote mbili zimekubaliana kuendeleza ushirikiano mzuri ambao umedumu kwa muda mrefu hususan katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuendelea kuimarisha uhusiano wa biashara kati ya pande mbili. Kupitia Waziri huyo Serikali ya Ufaransa imeahidi kuongeza kiwango cha fedha kwa ajili ya ufadhili wa miradi ya maendeleo katika sekta ya miundombinu, kilimo, afya na maji.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Samwel Shelukindo, Katibu Mkuu wizara ya Afya – Idara kuu ya maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk N Mbarouk.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...