Na Jane Edward,Arusha

Baadhi ya wakandarasi wa umeme zaidi ya hamsini wamepatiwa semina na shirika la umeme Tanzania (Tanesco) ya matumizi ya mfumo mpya unaojulikana kwa jina la NIKONEKT lengo likiwa ni kuwezesha huduma hiyo kufanyika kidigitali.

Akizungumza na wakandarasi hao jijini Arusha, Meneja wa Tanesco Mkoa Mhandisi Herini Muhina amesema mfumo huo umekuja kama mkombozi kati ya wateja na watoa huduma za nishati ya umeme.

Ameongeza kuwa mfumo huo wa Nikonekt utawezesha kutatua changamoto za wateja zilizokuwa zinatokea za kutapeliwa na vishoka na kusababisha kupata hasara kubwa, na hivyo kuingia kwenye mfumo huo utamrahisishia mteja kufatilia kazi yake kwa kupitia simu ya mkononi.

Amesema kwa sasa hapa nchini mfumo huo unatumika zaidi Mkoa wa Dar es salaam na Pwani na kwamba kwa Kanda ya kaskazini ndyo umeingia rasmi na utaanza kutumika kuanzia tarehe 30 .

Kwa upande wake meneja wa Ewura Mkoa wa Arusha Lorivii Longidu amewapongeza Tanesco kwa kuja na mfumo huo wa Nikonekt na kwamba utapunguza utapeli waliokuwa wakifanyiwa wateja na kusababisha malalamiko mengi na wao kama Ewura wako tayari kushirikiana na Tanesco katika utoaji wa elimu hiyo endelevu.

Nao baadhi ya wakandarasi hao waliopatiwa semina hiyo Bosco Mwamba ameishukuru Tanesco kwa kuwapa elimu ya matumizi ya mfumo huo na kuahidi kuwa watautumia kwa uaminifu na kuondoa malalamiko kati ya mafundi na wateja.

Amebainisha kuwa baada ya semina hiyo wao watakuwa mabalozi wa kuhakikisha wenzao nao wanapata elimu hiyo na kuwataka Tanesco kutoishia hapo tu waite mafundi wengine ili elimu iendelee kusambaa zaidi ili kupunguza Changamoto zilizokuwa zinajitokeza.


Meneja wa Ewura Lorivii Longidu Akizungumzia nafasi ya Ewura katika huduma hiyo ya Nikonekt.
Meneja wa Tanesco Arusha mhandisi Herini Muhina akitolea ufafanuzi huduma ya Nikonekt.
Afisa mahusiano Tanesco Arusha Vesso Kuppa akizungumza na wakandarasi hao pichani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...