Wakati maonyesho ya madini
yakifikia ukingoni kampuni ya uuzaji wa mitambo ya magari ya mizigo Gf
Trucks & Equipment iliandaa semina elekezi kwa ajili ya wachimbaji
wa madini na viongozi wa chama cha wachimbaji madini yenye lengo la
kuwajengea uwezo
Maonyesho hayo ambayo kwa mara ya kwanza
yamefanyika wilayani Chunya mkoani Mbeya, yamefungua fursa kwa
wafanyabiashara katika sekta hiyo ya madini kukutana na kuweza
kubadilishana uzoefu kwani katika maonesho hayo ya makampuni tofauti
nchini yalishiriki na kubadilishana uzoefu na wachimbaji hao.
Akizungumza
wakati wa semina elekezi Meneja Masoko na Mawasiliano wa kampuni ya GF
Trucks ,Smart Deus alisema wachimbaji wengi wanauwezo wa kununua na
hata kukodisha mitambo ya huduma ambayo inapatikana katika kampuni yetu
ya GF lakini tatizo kubwa hawana uelewa wa kutosha katika uendeshaji
kazi, ambayo anaachiwa opareta wa mashine wakati mwingine anaweza
kumuongopea bosi kuwa Mtambo unatumia mafuta mengi kumbe ni si kweli,
sasa kupitia semina hii tumewaeleza namna bora ya kuitunza mitambo ili
iweze kudumu muda mrefu na kuepukana na matatizo yanayoweza kuzuilika
Gf
kwa sasa imefungua kiwanda cha kutengeneza maroli ya GFA kilichopo
Kibaha mkoani Pwani kwa kutanua na kutumia magari ya FAW unaliongezea
Taifa fedha, kwani magari hayo yanatengenezwa nchini kwetu na sisi
tunajivunia cha kwetu.
Pia GF hivi karibuni itafungua ofisi
(yadi) katika mkoa wa Mbeya ili kuwasogezea huduma jirani wachimbaji
kutoka ukanda wa nyanda za juu kusini kwa hiyo wateja wa Njombe,Chunya
na Songwe wakae mkao wa kula wa kusogezewa huduma jirani hii ikiwa ni
kutii maagizo ya mkuu wa mkoa wa Mbeya aliyetutaka kusogeza jirani
huduma zetu.
GF pia ni wauzaji wa mashine za XCMG,AJAX, pamoja na maroli ya mizigo ya FAW na HONGYAN.
Akitoa
neno la shukrani Mwenyekiti wa Chama Cha Wachimbaji Madini mkoani Mbeya
(Mberema) Leonard Manyesha alisema anawashukuru GF kwa kuweza kuwapa
semina elekezi juu ya namna bora ya kutunza na kuisimamia mitambo yao
katika shughuli za uchimbaji iliiweze kudumu kwa wakati na kuepuka
kupata hasara zinazoweza kuzuilika Pia alisema wamefurahia kupata
utaratibu rafiki kwa kuweza kukopa mmitambo hiyo kupitia mmoja ya benki
kwa kutimiza mashari nafuu ambayo dhamana itakuwa mtambo wenyewe.
Meneja Masoko na Mawasiliano GF Trucks & Equipment, Smart Deus na Afisa Mauzo wa kampuni hiyo Peter Willium wakijadiliana jambo na viongozi wa Chama cha wachimbaji madini mkoa wa Mbeya (MBEREMA), upande wa kulia wakati wa semina ya namna bora wa kutumia mitambo ya XCMG na magari ya FAW kwa wachimbaji iliyofanyika Chunya mkoani Mbeya.
Mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini mkoa wa Mbeya(Mberema) ,Leonard Manyesha akipokea zawadi ya vifaa kutoka kwa Meneja Masoko na Mawasiliano GF Trucks & Equipment , Smart Deus kwa ajili ya kujikinga na vumbi pamoja na jua wawapo mgodini mara baada ya semina elekezi iliyooendeshwa na kampuni ya Gf wakati wa maonyeshobya madini yaliofanyika Chunya mkoani Mbeya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...