Na. Dennis Gondwe, CHAMWINO

KATA ya Chamwino yaadhimisha maadhimisho ya Siku ya Usafi Duniani kwa kufanya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya kata hiyo.

Akiongelea maadhimisho hayo, Afisa Mtendaji wa Kata ya Chamwino, Lucas Nkelege alisema kuwa maadhimisho hayo yamefanyika kwa kufanya usafi wa mazingira katika barabara inayotoka makutano ya Wajenzi mpaka kona ya Viva la vida. Alisema kuwa usafi huo ulihusisha kusafisha mtaro wenye urefu wa mita 1,500.

“Usafi wa mazingira pia ulifanyika katika mitaro yote inayozunguka Shule ya Sekondari ya Hijra na wananchi walijitokeza na kufanya usafi katika korongo karibu na uwanja wa Shell Complex. Zaidi ya kusafisha mitaro, usafi huo ulihusisha kutoa taka ngumu na kuokota makopo na mifuko kwenye mtaro na maeneo ya pembezoni mwa barabara na korongo” alisema Nkelege.

Akiongelea mafanikio ya maadhimisho Siku ya Usafi Duniani, alisema kuwa yametokana na ushirikiano wa karibu na wadau mbalimbali. “Napenda kutoa shukurani za dhati kwa uongozi wa Kituo cha vipaji cha Shell Sports chini ya Mwenyekiti, Abdallah Mohamed ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Chamwino, uongozi wa Shule ya Sekondari ya Hijra kwa namna wanavyozilea Club za Mazingira tangu kuanzishwa kwake kwa kuwajengea vijana wadogo moyo wa kushiriki mambo ya kijamii ikiwamo kudumisha usafi wa mazingira. Kwa uzito huohuo, shukrani ziende kwa maafisa, Ally Mfinanga, Melania Mtui na Hadija Nyamsingwa kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma walioshirikiana nasi katika kufanikisha maadhimisho haya” Nkelege.


Maadhimisho ya Siku ya Usafi Duniani mwaka 2023 yaliongozwa na kaulimbiu isemayo “Tuungane pamoja kujifunza, kupanga na kuhimiza uimarishaji huduma za taka”.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...