Njombe


Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ameagiza vyombo vya usalama mkoani humo kutimiza wajibu wao wa kwanza wa kulinda raia na mali zao ili kudhibiti vitendo vya wizi pamoja na matukio mbali mbali mkoani humo.

Mtaka ametoa agizo hilo mara baada ya kupokea maelekezo mbali mbali ya Chama wakati walipokuwa kwenye kikao cha halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Njombe kilichowajumuisha pia wataalamu mbali mbali wa serikali kutoka kwenye halmashauri za mkoa huo ambapo Mwenyekiti wa CCM Deo Sanga awali alielekeza serikali kuzitatua kero za wananchi kwa wakati pamoja na kudhibiti matukio ya ujambazi.

Awali Deo Sanaga alisema "Leo tumeona ni vizuri tumuagize mkuu wa mkoa ahakikishe anakwenda kusimamia jambo hili ikiwemo kero za ardhi mtaona wenyewe juzi watu wametoka sehemu mbalimbali wamevamia mkoa wetu lakini mkuu wa mkoa ameweza kukamata mtandao unaohusika na ujambazi"alisema Sanga

"Tuliwaambia wafanyabiashara wa Njombe wafanye biashara masaa 24 sasa hatuwezi kuwa na watu wanafanya biashara kwenye maduka halafu kuna mtu ana kwenda kuvamia,hatuwezi! hatutaweza kuvumilia jambo la kijinga namna hiyo tumeelekeza kila vyombo vichukue jukumu lake na haya mambo yote ya kijinga kuhusu uhalifu yataisha"amesema Mtaka

Nao baadhi ya wabunge wa mkoa wa Njombe akiwemo Deo Mwanyika,Joseph Kamonga na Edwirn Swalle wametoa wito kwa serikali kushughulikia changamoto ya uhaba wa mafuta ili kurahisisha usafirishaji wa mazao kutoka vijijini kwenye majimbo yao.

Naye katibu wa siasa na uenezi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Njombe Josaya Luoga amesema wanatarajia kwenda kwenye wilaya zote ili kukagua utekelezaji wa Ilani ambapo ametoa wito kwa watendaji kujiandaa wa halmashauri kujiandaa kwa ziara hiyo ya viongozi wa Chama.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya matukio ya wizi kutokea hivi karibuni mkoani humo na kusababisha taharuki kwa wananchi pamoja na majambazi kusababisha mauaji kwa lengo la kuhitaji fedha kwa wafanyabiashara wa kifedha.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...