NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WAPENDWA,
KWA MARA NYINGINE NAOMBA KUTUMIA NAFASI HII KWA NIABA YA FAMILIA YA MAZARA KATIKA KUTOA SHUKRANI ZETU ZA DHATI KWA USHIRIKIANO WENU MKUBWA MLIO UONYESHA KATIKA HATUA ZA MWISHO ZA KUMUAGA BINTI YETU SHEMSA KENNEDY MAZARA TULIYEMZIKA JUMAMOSI MCHANA YA TAREHE 30/06/07 HUKO DENTON DALLAS(USA).
KWA WALE MLIOFANIKIWA KUFIKA KATIKA MAZISH NA WENGI SANA AMBAO HAMKUWEZA KUFIKA KWA SABABU MOJA AU NYINGINE(IKIWA NI PAMOJA NA SUALA LA UMBALI) NI KWA NGUVU ZAKE MWENYEZI MUNGU, MAOMBI YENU NA PIA UPENDO WENU WA DHATI KWA MAREHEMU NA FAMILIA YAKE NDIYO ULIOWEZESHA SHUGHULI NZIMA KUFANIKIWA KWA KIASI KIKUBWA KIASI HICHO!!!!.
MICHANGO NA USHIRIKIANO WENU WA HALI NA MALI TUTAENDELEA KUIKUMBUKA SIKU ZOTE NA PIA KUWAOMBEA KWA MUNGU ILI AWAZIDISHIE.
Ni Wenu Katika Jina La Bwana.
Parobah Mazara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 03, 2007

    Poleni na msiba jamani. Nawapongeza kwa uamuzi wenu wa kumzika marehemu huko huko Dallas. Bila shaka mmebana matumizi kwa njia hiyo.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 03, 2007

    Kennedy Mazara & Family, our condolences on the passing of your daughter.

    Mungu amweke Shamsa mahali pema peponi.

    Jimmy & Lucy
    Dar-es-Salaam, Tanzania

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 06, 2007

    Nasi tunaungana na Watanzania wenzetu kutoa rambirambi kwa familia yote ya Mazara kwa msiba wa binti yetu Shamsa.

    Amani na faraja iwe nanyi nyote.

    Judy, Marja & Musuto Chirangi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...